WIRE โ€” Shangazi. Nina rafiki wa kiume ambaye tumejuana tangu chuo kikuu. Hakuna uhusiano wa kimapenzi kati yetu na mume wangu anamjua. Hata hivyo, baada ya rafiki huyo kunisaidia kupata nafasi ya kazi, mume wangu alianza kumshuku. Sasa anataka niache kabisa kuwasiliana naye. Anasema mwanaume na mwanamke hawawezi kuwa marafiki bila mmoja kuwa na nia tofauti. Mimi sitaki kumpoteza rafiki yangu, lakini pia sitaki ndoa yangu iwe na mashaka kila siku. Nimechanganyikiwa. Urafiki wa watu wa jinsia tofauti unawezekana, lakini mipaka yake lazima iwe wazi, hasa ndani ya ndoa. Jiulize kama mawasiliano yako na rafiki huyo yangeonekana ya kawaida iwapo mume wako angekuwa karibu. Epuka siri, mazungumzo ya usiku yasiyo ya lazima au ukaribu unaoweza kuonekana kama uhusiano wa kimapenzi. Wakati huo huo, mume wako hapaswi kutumia wivu kukutenga na kila mtu. Binti yangu anachafuka mno, ni kawaida? Nina binti wa miaka 15 ambaye ni mwerevu sana darasani lakini chumba chake kinaonekana kama eneo lililopigwa na kimbunga. Nguo ziko kila mahali, vitabu vimetapakaa na hata vikombe vya chai hukaa humo kwa siku kadhaa. Kila nikimwambia asafishe, anasema ataifanya baadaye lakini hachukui hatua yoyote. Nimeanza kuogopa kuwa tabia hii itamfuata hadi utu uzima. Nifanyeje? Vijana wengi hupitia Tatizo kama hilo. Badala ya kumfokea kila siku, msaidie kuona umuhimu wa usafi na mpangilio katika maisha ya kila siku. Weka matarajio ya wazi na majukumu maalum. Pia mfundishe kwa mfano badala ya maneno pekee. Usafi wa mazingira hujenga nidhamu, uwajibikaji na hata afya ya akili. Tabia hizi hujengwa taratibu kupitia mwongozo unaofaa. Mwanangu amekuwa mkora sana Nilianza kumpa mwanangu aliye chuoni pesa kila wiki kwa ajili ya chakula na usafiri. Baada ya muda niligundua kwamba baadhi ya matumizi aliyokuwa akiniambia hayakuwa ya kweli. Alikuwa akisema pesa zimetumika kununua vitabu, kumbe alikuwa akitumia sehemu yake kupiga sherehe. Nifanyeje. Uongo wake unapaswa kushughulikiwa, lakini lengo liwe kumfundisha uwajibikaji, si kumwangamiza. Mkae chini mtengeneze bajeti na umweleze wazi kiasi utakachompa na matumizi yanayotarajiwa. Badala ya kumtumia pesa bila mpango, unaweza kumshirikisha katika kupanga mahitaji yake. Pia mfundishe kuwa uhuru unaambatana na uwajibikaji. Akifanya makosa, lazima akabiliane na matokeo yake. N'nahofu kufika umri wa kuzeeka Shangazi, nimefikisha miaka 50 na nimeanza kuona mabadiliko mengi mwilini. Nguvu zimepungua na sura si kama zamani. Wakati mwingine nahisi kama thamani yangu inapungua kadri ninavyozeeka. Hali hii inanihuzunisha. Nifanyeje? Kuzeeka si adhabu bali ni zawadi ambayo wengi hawakupata. Uzuri wa ujana hupungua, lakini hekima, uzoefu na utulivu huongezeka. Angalia maisha uliyojenga, watu uliowagusa na changamoto ulizoshinda.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.