WIRE โ WANAFUNZI 2,400 kutoka eneo la Bisil, Kaunti ya Kajiado, watanufaika na vifaa vya usafi na elimu kuhusu afya kupitia mpango mpya unaolenga kuboresha usafi shuleni. Mpango huo, unaojulikana kama Clean Futures Alliance, umeanzishwa na Federal Express Corporation (FedEx) kwa ushirikiano na Feed the Children, huku ukilenga kuwasaidia watoto na vijana kujenga uzoefu wa kudumisha usafi kwa lengo la kuwalinda dhidi ya magonjwa. Kupitia mpango huo, wanafunzi wa shule za msingi watapokea vifaa vya usafi binafsi na kushiriki katika mafunzo yanayowafundisha umuhimu wa kunawa mikono, kudumisha usafi wa mwili na kuzingatia mazingira safi. Shughuli za kwanza za elimu kuhusu maji, usafi na usafi wa mazingira (WASH) zilifanyika katika Shule za Msingi za Inkati na Noontoto, Bisil. Kwa watoto wanaotumia muda mwingi shuleni, usafi ni sehemu muhimu ya maisha yao ya kila siku. Ukosefu wa vifaa au maarifa kuhusu usafi unaweza kuwaweka katika hatari ya kupata magonjwa na pia kuathiri masomo yao. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mkurugenzi Mkuu wa Operesheni za FedEx katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Nelson Teixeira, alisema kampuni hiyo inalenga Kumari Sha usafi katika jamii. "Tunataka kusaidia watoto na familia kujenga maisha yenye afya na kuleta mabadiliko katika jamii tunamoishi na kufanya kazi," alisema. Kwa upande wake, Rais na Afisa Mkuu Mtendaji wa Feed the Children, Emily Callahan, alisema usafi huwasaidia watoto kuwa na afya bora, kujiamini na kuendelea kushiriki katika masomo. Ushirikiano huo unatekelezwa kupitia mpango wa FedEx Cares, ambao huwahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo katika shughuli za kujitolea na miradi inayolenga kushughulikia mahitaji ya jamii. Mbali na kutoa vifaa, wafanyakazi wa FedEx walishiriki katika kuandaa na kusambaza vifaa vya usafi kwa wanafunzi. Mpango huo unatarajiwa kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya FedEx na Feed the Children katika kusaidia jamii kupata mahitaji muhimu na kujenga mazingira bora kwa watoto kukua na kusoma.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.