WIRE โ€” KENYA inajiandaa kuanza kuzalisha nishati kwa kutumia nuklia huku kiwanda chake cha kwanza cha nuklia kikipangiwa kuzinduliwa rasmi Machi, mwaka ujao. Machi 25, 2026, Rais William Ruto alitangaza kuhusu mpango wa nuklia nchini katika kongamano la kimataifa kuhusu Nishati ya Nuklia lililoandaliwa jiji kuu la Nairobi. Maandalizi sasa yameshika kasi Kenya ikijiandaa kuanzisha kiwanda chake cha kwanza cha nuklia. Mradi huo uliopendekezwa unakadiriwa kugharimu takriban Sh500 bilioni na umepangiwa kuzinduliwa katika kijiji cha Lenya, Kaunti ya Siaya, eneo lililotambuliwa kuwa mwafaka zaidi, kwa mujibu wa Taasisi ya Nishati na Kawi ya Nuklia (NuPEA). Mradi huo umekadiriwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027, ukitengewa mgao wa Sh80 milioni kufadhili shughuli za "Eneo la Kiwanda cha Kawi ya Nuklia," ikiwemo uhandisi na udadisi kiufundi, yanaashiria makadirio ya bajeti yaliyowasilishwa katika Bunge la Kitaifa. Hata hivyo, maswali tele yamezuka kuhusu Kenya ilivyojiandaa kuhakikisha usalama wa umma, manufaa kijamii, tishio kwa afya na mazingira kutokana na uzalishaji kawi kinuklia. Mwezi uliopita, wabunge na maseneta walitaka ufafanuzi wa kina kutoka kwa NuPEA, katika kikao cha Kamati ya Seneti kuhusu Kawi. Kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Siaya, Oburu Odinga ilihoji kuwa mchakato wa kutathmini eneo mwafaka pekee unaweza kuchukua karibu mwaka mmoja ikisaili tarehe ya uzinduzi. Seneta wa Kakamega Bonni Khalwale alisaili mikakati ya dharura inayohitajika kwa mradi kama huo ikiwemo kusaidia serikali ya Siaya kuanzisha Hospitali ya Level 5 na kuboresha miundomsingi kijamii. Mbunge wa Rarieda, Otiende Amollo alisisitiza haja ya kuangazia kikamilifu masuala ya kisayansi yanayohusiana na kawi ya nuklia, akisema bado hajajua eneo hasa la mradi huo. Alihoji kuwa mikakati ya kulinda mazingira ni sharti ipatiwe kipaumbele ikizingatiwa Ziwa Victoria linakidhi maelfu ya wanajamii eneo hilo. "Kihistoria, kawi ya nuklia haijahusishwa na matokeo bora. Masuala ya kisayansi yanahitaji kujibiwa kikamilifu," alisema Mbunge Amollo. Mkurugenzi wa NuPEA, Justus Wabuyabo aliwahakikishia kwamba sekta ya nuklia duniani imeboresha mikakati yake ya usalama. Alisema Kenya imepiga hatua kupitisha mikataba minne ya kimataifa kuhusu usalama wa nuklia iliyoidhinishwa na Baraza la Mawaziri Juni 30,2026, akifichua kuwa taasisi hiyo inasubiri uamuzi wa Bunge la Kitaifa. "Leo hii, kiwanda cha nuklia hakiwezi kuvuja kwa sababu ya mikakati ya usalama iliyowekwa," alisema Bw Wabuyabo.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.