WIRE โ€” KUKANUSHA ni kukataa, kukana, kutokubali au kupinga jambo fulani. Ili mwanafunzi akanushe sentensi kwa usahihi anafaa kuelewa hali na nyakati mbalimbali. Iwapo kukanusha viambishi vya nyakati na hali katika sentensi ni rahisi, baadhi ya wanafunzi huwa na changamoto wanapokanusha vitenzi vya silabi moja - kuja, kula, kufa na kunywa katika wakati uliopita. Aghalabu utapata sentensi kama vile: Watoto wale walikuja kwetu jana, ikiwa imekanushwa hivi: *Watoto wale hawakukuja kwetu jana. Ukanusho wa sentensi hii si sahihi. Silabi ku- imeongezwa katika kukanusha kitenzi walikuja. Ili kuisahihisha sentensi hiyo ifaavyo tunafaa kusema: Watoto wale hawakuja kwetu jana. Kosa hilo pia huwa la kawaida katika kukanusha kitenzi kula. Utapata sentensi: Wageni hao walikula matunda yote imekanushwa hivi: *Wageni hao hawakukula matunda yote. Ukanusho sahihi ni: Wageni hao hawakula matunda yote. Baadhi ya wanafunzi pia hupata changamoto wanapokanusha sentensi zenye vitenzi kufa na kunywa wakati uliopita. Mara kwa mara utapata sentensi kama vile: Wanyama wao walikufa wakati wa kiangazi. Mtoto wangu alikunywa chai, imekanushwa kwa kusema: *Wanyama wao hawakukufa wakati wa kiangazi. *Mtoto wangu hakukunywa chai. Ukanusho sahihi wa sentensi hizo ni: Wanyama wao hawakufa wakati wa kiangazi. Mtoto wangu hakunywa chai. Mwanafunzi mwenye changamoto katika kukanusha sentensi zenye vitenzi kula, kuja, kufa na kunywa katika wakati uliopita, anafaa kufanya mazoezi ya kuvitumia vitenzi hivyo kutunga sentensi katika wakati uliopita na kuzikanusha.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.