WIRE โ€” ZAIDIย ya miaka 10 tangu ujenzi wake uanze na karibu Sh300 milioni za walipa ushuru kutumika, makazi rasmi ya Gavana wa Turkana bado hayajakamilika huku mkandarasi wa pili akiondoka kwenye mradi huo. Kutokana na hali hiyo, gavana wa kaunti hiyo anaendelea kuishi katika makazi yake binafsi huku mradi uliotarajiwa kuwa moja ya mikubwa ya kaunti ukibaki kuwa ndoto. Ujenzi wa makazi hayo ulianzishwa mwaka wa 2015 wakati wa utawala wa gavana wa kwanza wa Turkana, Josphat Nanok. Hata hivyo, mradi huo umecheleweshwa mara kwa mara baada ya kampuni ya Landmark Holdings Limited, iliyopewa kandarasi mwaka wa fedha wa 2019/2020, kusitisha kazi ikidai haijalipwa fedha zake kwa wakati. Afisa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa Kaunti ya Turkana, Winston Ebei, alisema serikali ya kaunti imeanza rasmi mchakato wa kuvunja mkataba na kampuni hiyo baada ya kuomba kujiondoa kwenye mradi. "Kwa kushirikiana na Ofisi ya Gavana na Timu ya Utekelezaji wa Miradi ya Kaunti, tulikagua eneo la ujenzi kubaini kazi iliyokamilika na ile ambayo bado haijafanywa," alisema. Kulingana na rekodi zilizowasilishwa mbele ya Kamati ya Seneti ya Hesabu za Serikali za Kaunti, mkandarasi wa kwanza alilipwa Sh206 milioni kwa kazi ya msingi na sehemu ya majengo. Baadaye mkandarasi mwingine alipewa kandarasi ya Sh90.5 milioni kukamilisha kazi iliyobaki. Hata hivyo, naye alisimamisha ujenzi akidai malipo ya Sh28 milioni ambayo hayakuwa yametolewa. Mwaka wa 2023, Kamati ya Seneti ya Hesabu za Serikali za Kaunti ilipotembelea eneo hilo, ilieleza wasiwasi kuhusu kiwango kikubwa cha fedha kilichotumika ikilinganishwa na kazi iliyofanywa.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.