WIRE โ WANASIASA wengi nchini huchora taswira ya watu wasioweza kutikiswa kutokana na mamlaka wanayoshikilia, misafara ya magari, walinzi na bajeti kubwa wanazosimamia. Lakini hali hubadilika. Matatizo ya kifedha sasa yameanza kuwakumba baadhi ya viongozi wakuu huku benki zikielekeza madalali kuuza mali yao ili kufidia madeni. Aliyekuwa Gavana wa Murang'a na sasa mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Mwangi wa Iria, ndiye mwathiriwa wa hivi punde. Shirika la Dalali Traders Auctioneers limetangaza kuwa mnamo Agosti 25 litauza nyumba yake ya Karen pamoja na Hospitali ya Edinburgh Mountain na Chuo cha Edinburgh vilivyoko Murang'a kutokana na deni ambalo halijafichuliwa. Aliyekuwa Waziri Raphael Tuju ndiye mwanasiasa aliyepoteza mali nyingi zaidi mwaka huu. Mnamo Machi, alipoteza Dari Business Park iliyoko Karen baada ya Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) kuiuza kufidia mkopo wa dola milioni 9.3 (zaidi ya Sh1.2 bilioni) aliouchukua 2015. Deni hilo sasa limeongezeka hadi Sh4.5 bilioni. Wiki hii, kampuni ya Garam Investments ilitangaza pia mnada wa Entim Sidai Wellness Sanctuary, mali nyingine ya kifahari ya Tuju iliyoko Karen. Mfanyabiashara Mary Wambui Mungai, ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi ya Athi Water Works Development Agency, alipoteza hoteli yake ya Glee mwezi uliopita. Aliyekuwa Waziri Moses Kuria alinusurika kwa muda baada ya mkewe Joyce Njambi kupinga mpango wa Benki ya Equity kuuza majengo yao ya vyumba vya kupangisha yaliyoko Ruaka na Juja kufidia mkopo wa Sh54 milioni. Mkewe alidai mali hiyo ni ya ndoa na haikupaswa kutumika kama dhamana bila idhini yake. Kesi bado inaendelea mahakamani. Aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu pia amekuwa akipambana na wakopeshaji.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.