WIRE โ MABINGWA wa Ligi Kuu Uingereza (EPL) Arsenal, wamekubaliana na Newcastle United kuhusu uhamisho wa nahodha wao Bruno Guimaraes kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Uingereza zilizochapishwa Jumatano. Kwa mujibu wa Sky Sports, ofa ya kwanza ya Arsenal kwa kiungo huyo wa Brazil ilikataliwa mapema wiki hii. Hata hivyo, klabu hiyo ya London ilirejea na ofa iliyoboreshwa na kufikia makubaliano na Newcastle. Guimaraes sasa ameuzwa kwa Arsenal kwa ada ya pauni milioni 75 (Sh13.2 bilioni). Ripoti zinasema Guimaraes, 28, alikuwa ameiambia Newcastle kwamba angependa kujiunga na Arsenal iwapo ofa inayofaa ingewasilishwa. Newcastle ilikuwa ikitaka kusalia na nahodha huyo, ambaye bado ana miaka miwili katika mkataba wake, pamoja na mwanya wa kuongeza mwaka mmoja zaidi. Guimaraes alijiunga na Newcastle akitokea Olympique Lyon ya Ufaransa mnamo Januari 2022 na tangu wakati huo amekuwa nguzo muhimu ya klabu hiyo. Amecheza mechi 195 katika mashindano yote, akifunga mabao 31, na aliiongoza Newcastle kutwaa League Cup (Carabao 2025) taji lao la kwanza baada ya kipindi kirefu. Iwapo uhamisho huo utakamilika, Guimaraes ataongeza ubora na uzoefu katika safu ya kati ya kocha Mikel Arteta huku Arsenal ikisaka kutetea ubingwa wa EPL na pia kutamba katika Klabu Bingwa Ulaya (UEFA). Guimaraes pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil katika Kombe la Dunia 2026. Kuondoka kwake kutakuwa pigo jingine kwa Newcastle, ambayo tayari imewapoteza Anthony Gordon, Sandro Tonali na kocha Eddie Howe. Wakati huo huo, Kocha Mfaransa Herve Renard naye amerejea kuinoa Ivory Coast, miaka 11 baada ya kuiongoza kutwaa Kombe la Afrika 2015. Shirikisho la Soka la Ivory Coast lilitangaza Jumanne kuwa Renard, 57, atamrithi Emerse Fae, ambaye mkataba wake haukuongezwa baada ya Kombe la Dunia 2026. Fae alifikisha Ivory Coast hatua ya mchujo kwa mara ya kwanza katika kombe la dunia ambao walishiriki kwa mara ya nne. Renard aliinoa Tunisia kwa muda katika Kombe la Dunia baada ya kuanza vibaya kwa kipigo cha 5-1 dhidi ya Uswidi. Alishindwa kubadili mambo huku wakipoteza pia dhidi ya Japan na Uholanzi. Kocha huyo pia amewahi kuzinoa Angola, Morocco, Saudi Arabia na Zambia, aliyoiongoza kutwaa taji la AFCON 2012. Sasa atalenga kutwaa ubingwa wake wa tatu wa AFCON mwaka ujao katika mashindano yatakayoandaliwa kwa pamoja na Kenya, Tanzania na Uganda.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.