WIRE โ WASHINGTON, Amerika: UTAFITI mpya wa Reuters/Ipsos unaonyesha kuwa kwa mara ya kwanza katika karibu mwongo mmoja, raia wengi wa Amerika wanaamini Democrat ina uwezo mkubwa zaidi wa kusimamia uchumi kuliko Republican. Utafiti huo pia umebaini kuwa utendakazi wa Rais Donald Trump umeshuka hadi asilimia 35 na raia wengi wanaelekea kukosa imani naye kutokana na uchumi mgumu. Asilimia 37 ya wapigakura waliosajiliwa walisema Democrats wana sera bora za uchumi ikilinganishwa na asilimia 36 waliounga mkono Republicans, huku asilimia 27 wakisema hawakuwa na msimamo kuhusu Trump na utawala wake. Matokeo hayo yanakuja huku raia wa Amerika wakikabiliwa na kupanda kwa gharama ya maisha, wengi wakilalamikia pia mapato kidogo. La mno zaidi kwa raia wa Amerika ni kupanda kwa bei ya mafuta kutokana na vita kati ya Iran na Israel vinavyoungwa mkono na Amerika. Tangu vita hivyo vianze, bei ya petroli imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 25, jambo limeathiri pakubwa bajeti za familia nyingi na sekta za utengenezaji bidhaa. Kwa mujibu wa kura hiyo, asilimia 42 ya wapigakura wangewaunga wagombea wa Democratic iwapo uchaguzi wa Bunge ungefanyika sasa. Kwa upande mwingine asilimia 37 walisema wangewapigia kura Republicans. Wapigakura huru pia walionyesha kuwapendelea Democrats kwa tofauti ya asilimia 12 kuliko Republicans. Mwelekeo huo unaonyesha kuwa chama cha Republican kinachotarajia kutetea wingi wa wakilishi wake katika Bunge la Congress kwenye uchaguzi wa katikati ya muhula utakaofanyika Novemba, kina kibarua kudumisha umaarufu wake. Hata hivyo, wadadisi wa masuala ya kisiasa wameonya kuwa matokeo ya kura za maoni za kitaifa hayawezi kutabiri moja kwa moja matokeo ya uchaguzi kwa sababu ushindani mkali unatarajiwa katika idadi ndogo ya maeneo ya uchaguzi na si taifa lote. Rais Trump naye amepuuzilia mbali matokeo ya tafiti hizo, akidai kupitia mtandao wake wa Truth Social umaarufu wake upo juu zaidi kuwahi kushuhudiwa, na kwamba tafiti zinazochapishwa na vyombo vya habari hazionyeshi hali halisi. Amedai kuwa raia wengi wanachangamkia utawala wake na wana matarajio mengi kuwa serikali yake itaipaza Amerika kimaendeleo. Uungwaji mkono wa Republican kuhusu usimamizi wa uchumi umeendelea kupungua katika muhula wa sasa wa Rais Donald Trump, hasa baada ya bei ya mafuta kupanda kufuatia mashambulizi ya Amerika na Israel dhidi ya Iran mnamo Februari na vita vinavyoendelea.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.