WIRE โ€” RIPOTI ya siri ya polisi imefichua madai mazito ya ubakaji, ulawiti wa watoto na ukiukaji wa haki za kibinadamu unaodaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa kikosi cha Uingereza wanaopata mafunzo Kenya (BATUK) katika Kaunti ya Laikipia. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Mei 19, 2026, iliyotiwa saini na Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja na kuwasilishwa bungeni, baadhi ya wanajeshi walivuka kutoka eneo lao la mazoezi ya kijeshi hadi vijiji vya jirani na kuwashambulia wakazi. Katika kijiji cha Lekiji, Kaunti Ndogo ya Laikipia Kaskazini, msichana mwenye umri wa miaka 12 anaripotiwa kubakwa mara kadhaa na wanajeshi hao baada ya kushawishiwa kwa peremendepipi alipokuwa akivua samaki karibu na mto. Ripoti hiyo inadai kuwa baadaye alipata ujauzito na kujifungua mtoto mwenye asili mchanganyiko. Watoto wengine, kwa mujibu wa uchunguzi huo, walinaswa kwa kupewa biskuti, chokoleti na vinywaji kabla ya kudhulumiwa kingono. Ripoti hiyo inaeleza kuwa manusura wengi walitelekezwa wakiwa wamepoteza fahamu na kuokolewa baadaye na jamaa, majirani au wachungaji wa mifugo waliovutiwa na vilio vyao. Katika Kaunti ya Laikipia pekee, polisi walirekodi visa vya watu 37 waliodaiwa kubakwa na genge, watu 20 kubakwa na wengine wawili kujeruhiwa walipokuwa wakijaribu kutoroka mashambulizi hayo. Waathiriwa walieleza kuwa washambuliaji walikuwa wamevalia sare za kijeshi na mara nyingi waliwashambulia katika maeneo yaliyotengwa kama vichakani, njia za porini na kandokando ya mito walipokuwa wakichota maji, kukusanya kuni, kuogelea au kuchunga mifugo. Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa manusura wengi hawakupata matibabu hospitalini kutokana na hofu, unyanyapaa, mila za jamii na ukosefu wa huduma za afya. Badala yake, baadhi yao walifanyiwa matambiko ya jadi na kupewa dawa za mitishamba. Baadhi ya wanawake walidai walipoteza mimba baada ya mashambulizi hayo huku wengine wakisema hawakuweza tena kupata ujauzito. Wachunguzi walichukua taarifa kutoka kwa manusura 40 wenye umri kati ya miaka 48 na 90 waliotoa ushahidi kuhusu ukatili huo pamoja na madhara ya muda mrefu ya kimwili na kisaikolojia. Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa watoto waliozaliwa kutokana na visa hivyo wanakabiliwa na ubaguzi, unyanyapaa na kukosa msaada kutoka kwa wanaodaiwa kuwa baba zao. Polisi walitambua mtoto mmoja mwenye asili mchanganyiko Laikipia, huku ikielezwa kuwa sampuli za DNA za baadhi ya waathiriwa zilipelekwa Uingereza kwa uchunguzi kubaini baba mzazi. Kutokana na matokeo hayo, polisi wanapendekeza serikali ichukue hatua za kisheria kupitia mikataba ya kimataifa ya usaidizi wa kisheria na pia kuendelea na uchunguzi wa DNA kwa idhini ya waathiriwa ili kuwabaini wanaodaiwa kuwa baba wa watoto hao. Ripoti hiyo ilifuatia agizo la Bunge mwaka jana kwa polisi kufanya uchunguzi huru baada ya Kamati ya Ulinzi, Ujasusi na Mahusiano ya Kigeni kubaini madai ya unyanyasaji wa kingono, matumizi mabaya ya mamlaka na ukiukaji wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na wanajeshi hao. Wakati huo huo, licha ya serikali kutangaza kurejelewa kwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Kenya na Uingereza, wabunge wanataka makubaliano hayo yafanyiwe marekebisho ili kosa la mauaji lisikilizwe katika mahakama za Kenya na BATUK iwajibike zaidi kupitia miradi ya uwajibikaji kwa jamii.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.