WIRE โ€” KIGOGO wa Upinzani nchini Uganda Kizza Besigye alizirai Jumatano wakati akihudhuria kusikizwa kwa kesi yake jijini Kampala. Besigye, 70, amekuwa akikabiliwa na mashtaka ya uhaini tangu kunyakwa na maafisa wa Uganda akiwa ziarani Kenya karibu miaka miwili iliyopita. Alitiwa nguvuni pamoja na msaidizi wake Obeid Lutale Novemba 2024 jijini Nairobi. Walikanusha mashtaka na mawakili wao wametaja mashtaka hayo kuwa yaliyochochewa kisiasa. Majaribio kadhaa ya kuwaachilia yamezimwa na utawala wa Rais Yoweri Museveni na mwanawe mkuu wa jeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba. "Besigye aliziraiโ€ฆalikuwa amesimama halafu ghafla akaanguka. Baada ya muda, ambulansi ilikuja ikamchukua na kumpeleka tusikojua," Harold Kaija, afisa wa ngazi za juu katika chama cha Besigye cha PFF aliambia Reuters. SOMA PIA: Karua anyakwa na kuzuiliwa Uganda alikoenda kumwakilisha mwandani wa Besigye kortini Msemaji wa Magereza Frank Baine hakupokea simu alipopigiwa kutafuta maoni yake huku Msemaji wa Mahakama Ereemye Mawanda alisema hakuwa na uwezo wa kuzungumzia suala hilo kwa sababu hakuwa na habari kuhusu kisa hicho. Kuzuiliwa kwa Besigye kumekuwa kukiibua hasira za wanaharakati nchini humo na kimataifa huku Jumuiya ya Madola ikitaka aachiliwe huru. Mkenya mwanasiasa na wakili wa haiba ya juu Martha Karua alikuwa miongoni mwa utetezi wake kabla ya serikali kumzuilia katika uwanja wa ndege wa Entebbe na kumbadika kuwa 'mgeni asiyetakikana' Wakosoaji wa Museveni, 81, wanasema kuendelea kuzuiliwa kwa Besigye bila dhamana ni ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu na uwindaji wa wakosoaji nchini humo.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.