WIRE โ€” CHELSEA inaonekana kubadili mbinu yake ya usajili wa wachezaji baada ya kuelekeza macho kwa wachezaji wazoefu wenye umri uliokomaa. Hii ni baada ya klabu hiyo ya Stamford Bridge kutupia ndoano difenda wa Crystal Palace Maxence Lacroix, straika wa Brighton Danny Welbeck na kiungo wa kati wa Brentford Jordan Henderson. Hatua hiyo ni tofauti na mwelekeo waliochukua miaka minne iliyopita wa kusajili wachezaji chipukizi kwa mikataba mirefu. Baada ya klabu hiyo kununuliwa na BlueCo mwaka 2022, Chelsea ilitumia fedha nyingi kusajili nyota waliokuwa tayari wamejijengea majina makubwa. Raheem Sterling aliwasili kutoka Manchester City akiwa na miaka 27, Kalidou Koulibaly (31) alitua kutoka Napoli ya Italia huku Pierre-Emerick Aubameyang (33) akiingia kutokea Barcelona ya Uhispania. Lakini ukosefu wa mataji ulimgarimu kocha Thomas Tuchel kazi yake. Wakati wa kipindi kirefu cha uhamisho 2022 wamiliki wa BlueCo walipiga abautani kugeukia chipukizi. Aliyefungua ukurasa huo ni Enzo Fernandez kisha wakafuata mastaa wengine ikiwemo Moises Caicedo na Cole Palmer ambao wameonyesha ukwasi wao kwa kiwango fulani. Hata hivyo, kulikuwepo pia mastaa walioishia kuwa moto wa karatasi - Mykhailo Mudryk, Joao Feli na Wesley Fofana. Sasa baada ya miaka minne ya kukamata nafasi ya 12, sita, nne na 10 msimu jana pamoja na mataji 'madogo ya Conference League na Kombe la Klabu Bingwa Duniani, wamiliki wamegeukia tena mastaa wakongwe wenye uzoefu. Lacroix 26, ndiye mwenye umri mdogo kati ya watatu hao kwani Welbeck ana umri wa miaka 35 naye Henderson miaka 36. Chelsea inasemekana kuwa tayari kutoa Pauni milioni 52 (Sh9.2 billioni) kumsajili Lacroix. Naye Welbeck anaripotiwa kuwa tayari kujiunga na miamba hao kwani amebakisha mwaka mmoja pekee katika mkataba wake Brighton. Iwapo Welbeck atatua Chelsea huenda akachukua nafasi ya Liam Delap, 23, ambaye alisajiliwa kutoka Ipswich Town mwaka jana akiwa mmoja wa washambuliaji waliopigiwa upatu mkubwa kung'ara. Kocha mpya Xabi Alonso, ambaye amewasili kutoka Bayer Leverkusen ya Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), anasemekana kupendelea kikosi chenye mseto wa chipukizi na wazoefu. Sajili hizi kongwe zikifua dafu mashabiki wa Blues watasubiriwa kuona iwapo watawapaisha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu (EPL).

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.