WIRE โ TUME ya Huduma kwa Walimu (TSC) imetangaza nafasi 34,016 za kupandisha walimu vyeo katika shule za msingi, sekondari na vyuo vya mafunzo ya walimu. Waliopandishwa wapo katika madaraja 30, kuanzia Mwalimu Mkuu Mwandamizi II (Senior Teacher II) hadi Mkuu wa Shule (Chief Principal). Walimu wametakiwa watume maombi ya kazi hizo kupitia mtandao wa TSC kabla ya Agosti 10, 2026, huku TSC ikisisitiza kuwa maombi yanayowasilishwa moja kwa moja kupitia kwa mwalimu kufika na stakabadhi katika afisi za tume hayatakubaliwa. "Walimu wenye sifa zinazohitajika wanapaswa kutuma maombi yao kupitia tovuti ya TSC www.teachersonline.go.ke kabla ya Jumatatu, Agosti 10, 2026. Hakuna kuwasilisha stakabadhi katika afisi za TSC," ilisema TSC katika tangazo lake. Hatua hiyo inawapa matumaini walimu wengi ambao wamekwama katika madaraja yale yale kwa miaka mingi licha ya kutimiza masharti ya kupandishwa vyeo. Serikali imetenga Sh2 bilioni katika bajeti ya sasa kufanikisha shughuli hiyo. Hivi majuzi, TSC iliambia Bunge kuwa walimu 178,871 wa shule za msingi na upili wameendelea kubaki katika madaraja yao kutokana na uhaba wa fedha kwa muda mrefu. Walimu wengi waliokwama wako katika daraja la C3 kwa sekondari na C1 kwa shule za msingi. Kati ya nafasi zilizotangazwa, nyingi zinalenga madaraja ya kati ya taaluma. Kuna nafasi 13,490 za Senior Teacher II, nafasi 5,956 za Senior Master IV, na nafasi 4,210 za Senior Teacher I, ambazo zinatarajiwa kuwapa maelfu ya walimu nafasi ya kupanda vyeo. Tangazo hilo limekuja wakati Muungano wa Walimu wa Shule za Upili na Vyuo Anuwai (KUPPET) ukiendelea kushinikiza TSC kutangaza nafasi za kupandisha walimu 135,000 ambao wamekwama kwa muda mrefu katika madaraja yao ya kazi. Katibu Mkuu wa Kuppet, Akello Misori, alisema walimu wengi wamekuwa wakisubiri kupandishwa vyeo kwa miaka mingi licha ya kustahili. Kwa upande mwingine, wakuu wa shule kupitia chama cha KESSHA pia wameitaka TSC kuharakisha mchakato huo, wakisema walimu wakuu wengi hasa walio katika daraja la D3 wamevunjika moyo kwa kukosa nafasi za maendeleo ya kazi. Mwenyekiti wa TSC, Dkt Jamleck Muturi, alisema serikali imewapandisha vyeo walimu 274,285 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, lakini akakiri kuwa wengi bado wamekwama katika madaraja yao. TSC pia ilisema waliofaulu katika mahojiano watatakiwa kuwasilisha hati halali za zinazozingatia masharti ya Sura ya Sita ya Katiba kabla ya kuteuliwa rasmi, na watapangiwa shule ambako nafasi hizo zinapatikana.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.