WIRE โ€” KIVUMISHI ni neno linalotoa habari zaidi kuhusu nomino inayozungumziwa. Kuna aina mbalimbali kama vile: vivumishi vya pekee, vivumishi vya sifa, vivumishi viashiria, vivumishi vimilikishi, vivumishi vya idadi na vivumishi viulizi. Maneno safi, hodari na nadhifu ni vivumishi vya sifa ambavyo ni kapa au tasa. Vivumishi hivyo vinapotumiwa katika sentensi huwa havichukui viambishi vya nomino au vya ngeli yoyote. Kwa hivyo havibadiliki katika kuzungumzia nomino yoyote katika umoja au wingi. Ingawa vivumishi safi, hodari na nadhifu havifai kubadilika katika wingi au kuchukua viambishi vyovyote vya nomino, kuna mazoea ya wanafunzi kutunga sentensi kama vile: *Mwanafunzi mhodari katika somo la Kiswahili alituzwa jana. *Wakulima wahodari walipata mavuno mengi. Sentensi hizi si sahihi. Isitoshe, katika matumizi ya neno safi utakumbana na sentensi kama vile: *Vikombe visafi vimetumiwa kunywea chai. *Mwanafunzi msafi anavutia. Vilevile, kivumishi nadhifu hutumiwa isivyofaa kwa kutunga sentensi kama vile: *Wanafunzi wanadhifu walisifiwa na mwalimu.Mifano hii ya sentensi ina kosa la kuvipa vivumishi kapa safi, hodari na nadhifu viambishi. Ili kuzisahihisha tunafaa kusema: Mwanafunzi hodari katika somo la Kiswahili alituzwa jana. Wakulima hodari walipata mavuno mengi. Vikombe safi vimetumiwa kunywea chai. Mwanafunzi safi anavutia. Wanafunzi nadhifu walisifiwa na mwalimu. Mwanafunzi mwenye changamoto ya kutumia vivumishi safi, hodari na nadhifu kwa usahihi katika sentensi, anafaa kufanya mazoezi ya kutunga sentensi mbalimbali akitumia viumishi hivyo.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.