WIRE โ€” BAMBA, Kilifi: KIDOSHO aliyezaliwa na kulelewa mjini na kisha hivi majuzi kuolewa mashambani eneo hili alimwacha mama-mkwe, baba-mkwe na mashemeji zake wakishangaa. Hii ni baada ya kupatikana zizini akiwa amepakua sima kubwa kwenye bakuli na mboga akitembea zizini kuwalisha ng'ombe chakula hicho. Alipoulizwa na mavyaa kulikoni alidakia kwamba mumewe, ambaye alikuwa ameenda mjini, alimpigia simu kumwarifu kwamba masaa ya kulisha ng'ombe yalikuwa yamewadia. "Bwanangu amenijulisha kwamba niende kulisha ng'ombe kwani atarudi kuchelewa. Nimewapikia vizuri hii sima na mboga ili niwalishe washibe," akasema. Ni jibu lililomwacha mavyaa, bavyaa na mashemeji wakiangua kicheka wakijua fika kuwa muktadha wa 'kulisha ng'ombe' ulieleweka vibaya na kipusa huyo wa mjini, yaani born-tao au dotcom. Ilimlazimu mavyaa kumweleza mrembo huyo wa mjini kwamba kwenda kulisha ng'ombe hakukumaanisha kikweli kwamba alifaa kuwapikia chakula na kuwalisha mifugo hao kama alivyokuwa akifanya kwa wakati huo. "Jamani. Ulifaa kuwafungulia zizi uwapeleke kwenye nyasi wale. Huko ndiko kulisha mifugo na wala siyo kuwapikia na kuwalisha sima na mboga," akaeleza mavyaa huku akifululiza kicheko. Hata hivyo walimwelewa kutokana na kwamba amekuzwa mjini maisha yake yote na kwamba kuja kuishi kijijini ni jambo jipya kwake.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.