WIRE โ€” CHAMA cha Walimu wa Shule za Sekondari na Vyuo (KUPPET) kimepatia Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) siku 30 kurekebisha kasoro zinazokumba mpango wa matibabu wa walimu, kikionya kuwa kitachukua hatua ikiwa matatizo hayo hayatatatuliwa. KUPPET imeshutumu SHA kwa kushindwa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika taarifa mbili za pamoja zilizotiwa saini Machi 10 na Aprili 23, 2026, ambazo zililenga kuboresha huduma za afya kwa walimu. Katibu Mkuu wa Kuppet Akello Misori alisema tayari chama hicho kimeandikia SHA kutaka hatua za haraka zichukuliwe. "Siku hizi 30 zinatosha kutathmini hali ilivyo na kuamua hatua tutakazochukua ikiwa hakuna mabadiliko," alisema Bw Misori. Onyo hilo linajiri miezi mitatu baada ya SHA na KUPPET kukubaliana kuhusu hatua za kuboresha huduma za afya kufuatia malalamishi ya walimu kuhusu kucheleweshwa kwa matibabu na mapungufu katika utoaji wa huduma.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.