WIRE โ€” Kesi ya mauaji ya mwalimu na mwanablogu Albert Ojwang iliendelea Jumatano huku mpelelezi wa Mamlaka Huru ya Kusimamia Utendakazi wa Polisi (IPOA) akielezea mahakamani matukio ya mwisho kabla ya kifo chake. Akitoa ushahidi mbele ya Jaji Diana Kavedza-Mochache, afisa wa IPOA Joshua Mutua alisema Ojwang alifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Central mnamo Juni 7, 2025, saa tatu na dakika ishirini na tatu usiku, akiwa anatembea bila kusaidiwa na akionekana kuwa katika hali nzuri. Picha za kamera za CCTV zilizoonyeshwa mahakamani zilimuonyesha akisindikizwa na maafisa sita wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) waliokuwa wamefika kwa gari jeusi. Aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Central Samson Tallam, pamoja na maafisa James Mukhwana na Peter Kimani, wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya Ojwang. Wameshtakiwa pamoja na aliyekuwa afisa wa Kikosi cha Kukabiliana na Fujo (GSU) John Ngige Gitau, Gin Ammitou Abwao, na Brian Mwaniki Njue. Mahakama ilielezwa kuwa kabla ya kusajiliwa kituoni, Ojwang alionekana akipiga simu kadhaa. Baadaye maafisa wawili wa DCI walimsindikiza hadi ofisi ya kuripoti, ambako alikaa kwa takriban dakika 15. Wakati huo, maafisa Mukhwana na Kimani walinaswa na kamera wakizunguka ndani ya kituo huku wakipiga simu mara kadhaa. Baadaye mwanaume mmoja aliwasili kwa pikipiki, akaingia kituoni na kujiunga na maafisa hao wawili. Picha hizo zilionyesha Ojwang akisindikizwa hadi katika moja ya seli za mahabusu. Muda mfupi baadaye, Abwao na wanaume wengine wawili waliokuwa wameficha nyuso zao kwa kofia waliingia eneo hilo. Baadaye wanaume wanne walionekana wakimhamisha Ojwang kwa nguvu kutoka seli moja hadi nyingine. Mahakama pia iliona picha zikionyesha Mukhwana na Kimani wakibadilisha sare za polisi na kuvaa nguo za kiraia. Mwanaume mwingine alionekana akining'iniza blanketi kwenye mlango wa seli, jambo lililoonekana kuziba kuonekana ndani. Video hiyo pia ilimuonyesha mwanaume akiingia mara kwa mara chooni kuchota maji kabla ya kurejea katika seli aliyokuwa amewekwa Ojwang. Alifanya hivyo mara mbili kabla ya kutoka pamoja na wengine. Mmoja wao alionekana akichunguza kilichoonekana kuwa damu mkononi mwake. Majira ya saa saba na dakika kumi na nane usiku, Mukhwana na Kimani walivaa tena sare zao za polisi huku mwanaume aliyekuwa amewasili kwa pikipiki akiondoka kituoni. Muda mfupi baadaye, Kimani, Mukhwana na maafisa wengine wawili walinaswa wakimbeba Ojwang kutoka kwenye seli. Tallam alionekana akitangulia mbele walipokuwa wakimpeleka kwenye gari la polisi aina ya Land Cruiser. Walimpeleka katika Hospitali ya Mbagathi, walikofika saa saba na dakika hamsini na tisa usiku. Picha za CCTV za hospitali zilionyesha maafisa watatu wa polisi wakimtoa Ojwang, ambaye hakuonekana kuwa hai, kutoka garini, wakamweka kwenye machela na kumpeleka katika kitengo cha dharura. Mahakama ilielezwa kuwa maafisa hao hawakuonekana kuwa na haraka. Dakika chache baadaye, saa nane na dakika kumi na moja usiku, walimrudisha kwenye gari la polisi na kuondoka hospitalini

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.