WIRE โ WABUNGE wanataka makurutu 18 wa kike wa polisi waliofukuzwa katika Chuo cha Polisi Kiganjo mwezi Mei kwa sababu ya ujauzito warejeshwe mafunzoni baada ya kujifungua. Wanasema hatua hiyo ni ya ubaguzi kwa kuwa wanawake hao pekee waliadhibiwa ilhali wanaume waliowapa ujauzito waliendelea na mafunzo bila kuchukuliwa hatua. Mwakilishi wa Kike wa Makueni Suzanne Kiamba aliambia Bunge kuwa kufukuzwa kwa wanawake hao kunakiuka Kifungu cha 27 cha Katiba kinachohakikisha usawa wa wanawake na wanaume. "Hatua hiyo imeibua wasiwasi kuhusu kufuatwa kwa Katiba, sheria za ajira na kanuni za utawala wa haki," alisema. Suala hilo sasa linachunguzwa na Kamati ya Bunge kuhusu Utawala na Usalama wa Ndani inayoongozwa na Mbunge wa Narok Magharibi Gabriel Tongoyo. Kamati hiyo itachunguza msingi wa kisheria uliotumika kuwafukuza wanawake hao, iwapo walipewa nafasi ya kujitetea na hatua zinazochukuliwa kuwawezesha kurejea mafunzoni baada ya kujifungua. Mbunge wa Dagoretti Kaskazini Beatrice Elachi alihoji kwa nini wanawake pekee ndio wanaoadhibiwa. "Hauwezi kumfukuza mwanamke pekee. Vipi kuhusu aliyempa ujauzito?" alihoji.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.