WIRE โ KAULI ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ya kuwataka watalii na wawekezaji wa kigeni kusubiri hadi baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2027 kabla ya kuja Kenya imesolewa vikali serikalini, sekta ya utalii na hata baadhi ya washirika wake wa kisiasa. Akizungumza katika ibada ya kanisani mwishoni mwa wiki, Bw Gachagua alisema hali ya usalama nchini imezorota kutokana na ongezeko la ghasia za kisiasa na shughuli za makundi ya wahuni, akidai kuwa watalii na wawekezaji hawako salama. Kauli hiyo ilipingwa na Msemaji wa Serikali Isaac Mwaura, ambaye alisema utalii ni nguzo muhimu ya uchumi. Wakati huo huo,ย Rais William Ruto amekosoa Mahakama kwa kile alichosema ni kuwapa dhamana nafuu washukiwa wa uhalifu wanaotuhumiwa kuvuruga mikutano ya kisiasa, akisema hatua hiyo imechangia ongezeko la wahuni nchini. Akizungumza Ikulu, Nairobi, Jumanne, Rais alisema washukiwa wanaokamatwa kwa makosa ya jinai huachiliwa kwa dhamana ndogo na kurejea mitaani kuendelea na vitendo vyao. "Vijana wanaokamatwa kwa uhalifu hupelekwa mahakamani, wanapewa dhamana ya Sh200 na kuachiliwa kwa sababu ni watoto wetu. Kisha wanarudi katika mikutano ya kisiasa na kuendelea na vitendo vya kihuni," alisema Rais Ruto. Alisema Kenya lazima iwe na mjadala wa dhati kuhusu ongezeko la wahuni huku joto la kisiasa likizidi kupanda kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amesema uchunguzi unaendelea kubaini waliohusika na vurugu hizo.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.