WIRE โ€” ENEO la Pwani limezidi kubaki nyuma katika uzalishaji wa chakula, licha ya uwekezaji wa mabilioni ya pesa katika mifumo ya kilimo cha unyunyizaji maji shambani katika kaunti mbalimbali za ukanda huo. Katika Kaunti ya Taita Taveta, mifumo ya unyunyizaji ambayo hapo awali iliifanya Taveta kuwa miongoni mwa maeneo muhimu ya uzalishaji wa chakula kufaa Mombasa, Nairobi na Tanzania imeathiriwa na mifereji iliyozibwa na tope, magugu na uchafu, pamoja na kupungua kwa maji katika mito. Serikali ya Kaunti ya Taita-Taveta imekiri kuwa changamoto za usimamizi, mabadiliko ya tabianchi, uwekezaji duni na miundombinu chakavu imepunguza uzalishaji katika kilimo. Hata hivyo, kaunti inapanga kufufua mifumo ya unyunyizaji na kuwahamasisha vijana kuchukulia kilimo kama taaluma yenye faida. "Ukosefu wa rasilimali za kutosha umeathiri ukarabati wa mifumo ya unyunyizaji. Wakati huo huo, vijana wengi wameacha kilimo kwa sababu wanataka mapato ya haraka katika sekta ya bodaboda," akasema Waziri wa Kilimo katika kaunti hiyo, Bw Dawson Mzenge. Wakati huo huo, mfereji wa Njoro Kubwa, unaohudumia zaidi ya miradi 10 ya unyunyizaji, haujasafishwa kwa karibu miaka miwili. Hali hiyo imepunguza mtiririko wa maji na kuwaathiri mamia ya wakulima. Katika Kaunti ya Tana River, Miradi ya Unyunyizaji ya Bura na Hola nayo inakabiliwa na changamoto za miundomsingi na upatikanaji wa maji. Bura, iliyoanzishwa mwaka wa 1978, ina eneo lililotengwa la hekta 176,000, lakini ni karibu ekari 12,000 pekee zilizo na miundomsingi bora ya unyunyizaji. Serikali imetumia zaidi ya Sh7 bilioni katika mpango wa kuifufua Bura na kubadilisha mfumo kutoka pampu zinazotumia mafuta ya dizeli hadi mfumo wa maji yanayotiririka kwa nguvu ya mvuto asili. Mamlaka ya Kitaifa ya Unyunyizaji inasema mfereji wa kilomita 26 umekamilika na umeongeza upatikanaji wa maji huku ukipunguza matumizi ya dizeli. Katibu wa wizara kuhusu unyunyizaji, Bw Ephantus Kimotho, alisema mfumo mpya ni hatua muhimu ya mabadiliko. "Mradi unakusudia kuondoa gharama kubwa ya kutegemea mafuta kwa unyunyizaji ili uwezo wa unyunyizaji utumike kikamilifu," alisema alipozuru eneo hilo hivi majuzi. Alisema uwekezaji zaidi katika unyunyizaji utaongeza uzalishaji wa kilimo, kuunda ajira na kuimarisha upatikanaji wa chakula nchini. Maafisa wa Serikali pia wameeleza kuwa kuna ongezeko la wawejezaji binafsi wanaotaka kuwekeza katika miradi ya unyunyizaji. Katika mradi wa Bura, kuna mwekezaji anayehusika katika uzalishaji wa miwa ya mbegu katika eneo la ekari 700. Majaribio hayo yanahusisha aina nane za miwa kwa lengo la kubaini aina zinazofaa zaidi kwa eneo hilo. Serikali inaamini kuwa ubia kama huo unaweza hatimaye kuibadilisha Bura kuwa kitovu cha kilimo na viwanda chenye shughuli nyingi. Huko Kwale, sehemu ya umwagiliaji ya mradi wa Sh20 bilioni wa Bwawa la Mwache ilifutwa baada ya tathmini kuonyesha kuwa gharama za kusukuma maji ingekuwa kubwa na isiyo endelevu. Mradi huo sasa unaelekezwa zaidi kwenye unyunyizaji unaolenga wakulima wadogo karibu 2,000.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.