WIRE โ€” AFRIKA inapaswa kuendelea kuwekeza katika ubunifu wa kilimo na kuharakisha matumizi ya teknolojia zilizothibitishwa ili kuongeza kiwango cha uzalishaji wa chakula, kupunguza uagizaji wa vyakula kutoka nje na kujenga mifumo imara ya chakula inayostahimili athari za mabadiliko ya tabianchi. Wito huo ulitolewa wakati wa mkutano wa Harvesting the Future Africa Summit uliofanyika Nairobi mwezi Juni mwaka huu, 2026, ambapo viongozi wa serikali, taasisi za utafiti, sekta binafsi, mashirika ya maendeleo na wafadhili walisisitiza umuhimu wa kupeleka teknolojia zilizofanikiwa kwa wakulima wengi badala ya kusalia katika hatua ya utafiti. Mkutano huo uliandaliwa na Kituo cha Kimataifa cha Uboreshaji wa Mahindi na Ngano (CIMMYT) pamoja na washirika wake wakati ambapo sekta ya kilimo barani Afrika inakabiliwa na ukame wa muda mrefu, gharama za juu za uzalishaji, changamoto za upatikanaji wa mbolea, migogoro na kuyumba kwa uchumi. Mkurugenzi Mkuu wa CIMMYT, Bram Govaerts, alisema lengo ni kuhakikisha ubunifu wa kilimo unachangia usalama wa chakula, ajira na ukuaji wa uchumi. "Teknolojia zilizofanikiwa zinapaswa kuwafikia wakulima wengi na kwa haraka zaidi," akasema. [caption id="attachment_190349" align="aligncenter" width="300"] Mtambo wa kuosha maparachichi kwenye kiwanda. Picha|Sammy Waweru[/caption] Naye Dkt Agnes Kalibata, mwanachama wa Bodi ya CIMMYT, alisema Afrika tayari ina mifano mingi inayoonyesha jinsi sayansi inavyoweza kuongeza uzalishaji wa kilimo, lakini wadau wanahitaji kupewa raslimali za kutosha ili kufanikisha juhudi hizo. "Kinachohitajika zaidi ni raslimali kuonyesha sayansi na teknolojia zinafanya kazi," Agnes akapendekeza. Washiriki wa mkutano huo wa Harvesting the Future Africa Summit walitaja mbegu bora, mbinu za kilimo himilivu kwa tabianchi, teknolojia za kuboresha afya ya udongo, huduma za ushauri wa kidijitali na mifumo bora ya mbegu kuwa miongoni mwa ubunifu unaowasaidia wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi huku wakiongeza mavuno na mapato. Aidha, walieleza kuwa kuimarisha sekta ya kilimo kutasaidia kuzalisha ajira, kupunguza utegemezi wa uagizaji wa chakula na kukuza uchumi wa nchi za Afrika. Ripoti ya hivi majuzi ya uchambuzi wa mifumo ya chakula inaonyesha Kenya inakabiliwa na upungufu wa mayai bilioni tano, lita bilioni 6.5 hadi 7.5 za maziwa, tani 340,000 za samaki na tani 5,500 za asali kila mwaka. [caption id="attachment_190350" align="aligncenter" width="300"] Avokado kwenye kiwanda. Picha|Sammy Waweru[/caption] Ripoti hiyo iliyofadhiliwa na Financial Sector Deepening Kenya (FSD Kenya) chini ya mradi wa Green Finance for Youth Employment (GFYE) na kutolewa Mei 2026, inadokeza kuwa Kenya hutumia kati ya Sh288 bilioni na Sh500 bilioni kuagiza chakula kutoka nje kila mwaka. CIMMYT inasisitiza kuwa ushirikiano kati ya serikali, taasisi za utafiti, kampuni za mbegu, mashirika ya wakulima na washirika wa maendeleo ni muhimu ili kuhakikisha teknolojia zinazobuniwa zinawafikia wakulima na kuongeza uzalishaji wa chakula barani Afrika.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.