WIRE โ BAADA ya kuibuka mabingwa wa bara Ulaya miaka miwili iliyopita jijini Berlin huko Ujerumani, Uhispania walitawazwa wafalme wa dunia mnamo Jumapili usiku baada ya kukomoa Argentina 1-0 katika fainali ya Kombe la Dunia huko New Jersey, Amerika. Walipata tena mafanikio kama hayo mnamo 2010, miaka miwili baada ya kushinda Euro 2008. Ufanisi wa hivi punde wa Uhispania unaendeleza ubabe wao katika soka ya wanaume na wanawake. Ndilo taifa la kwanza kutwaa Kombe la Dunia la wanaume na wanawake kwa wakati mmoja. Vipusa wao walicharaza Uingereza 1-0 katika fainali ya Kombe la Dunia huko Sydney, Australia mnamo 2023. Wanaume wao nao walishinda Nations League mnamo 2023 na kuzoa nishani ya dhahabu katika Olimpiki ya 2024 huku wanawake wakinyanyua Nations League mnamo 2024 na 2025. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Uhispania sasa wametia kibindoni mataji 16 ya mashindano ya soka ya haiba kubwa duniani na bara Ulaya kuanzia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 hadi kiwango cha juu. Isitoshe, hawajafungwa katika mechi 38 zilizopita katika mashindano yote, rekodi ambayo ni ndefu zaidi kuwahi kuwekwa na timu yoyote ya bara Ulaya au Amerika Kusini katika historia. Argentina waliokuwa mabingwa watetezi walipiga jumla ya pasi 464 pekee ikilinganishwa na 852 za Uhispania. Emiliano Martinez wa Argentina alilazimika kuokoa jumla ya makombora 11, idadi ya juu zaidi ya makombora ambayo kipa yeyote amewahi kuzuia na kupangua katika fainali ya Kombe la Dunia. Kylian Mbappe ndiye mchezaji wa kwanza kushinda Kiatu cha Dhahabu cha Kombe la Dunia mara mbili mfululizo baada ya kuibuka mfungaji bora wa makala ya 2026. Fowadi na nahodha huyo wa Ufaransa alifunga mabao 10 katika mechi nane na kumpita Lionel Messi wa Argentina aliyepachika wavuni mabao manane. Mbappe, 27, alishinda Kiatu cha Dhahabu katika Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar baada ya kufunga mabao manane. Ndiye sogora wa kwanza baada ya Gerd Muller wa Ujerumani mnamo 1970 kufunga mabao 10 katika makala moja ya Kombe la Dunia. Just Fontaine, ambaye alifunga mabao 13 akiwa na Ufaransa mnamo 1958, na Sandor Kocsis wa Hungary aliyepachika magoli 11 mnamo 1954, ndio wanaojivunia kufunga idadi kubwa zaidi ya mabao katika makala moja ya Kombe la Dunia. Mbappe pia sasa ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Kombe la Dunia kwa upande wa wanaume, akijivunia mabao 22, moja zaidi kuliko Messi. Wanasoka wa Uhispania walizoa tuzo zote zingine zilizosalia, ikiwa ni pamoja na nahodha wao Rodri kutuzwa Mpira wa Dhahabu kwa kuibuka Mchezaji Bora, Unai Simon kuwa Kipa Bora na Pau Cubarsi kutawazwa Chipukizi Bora wa Kombe la Dunia la 2026. Akiwa na umri wa miaka 19 na siku sita, Lamine Yamal ndiye mchezaji wa tatu mchanga zaidi kuwahi kucheza fainali ya Kombe la Dunia, baada ya Pele wa Brazil mnamo 1958 na Giuseppe Bergomi wa Italia mnamo 1982. Yamal sasa ndiye sogora wa tatu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kunyanyua Kombe la Dunia. Uhispania walipomteua Luis de la Fuente kuwa kocha wao mnamo Disemba 2022, wachache walitarajia kwamba angetwaa Nations League (2023), Euro (2024) na Kombe la Dunia (2026) ndani ya kipindi cha muda mfupi sana. Kuajiriwa kwake kulifanyika pindi baada ya Uhispania kubanduliwa na Morocco kwenye hatua ya 16-bora ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar na Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF) lilihitaji kujaza pengo lililoachwa wazi na mkufunzi Luis Enrique aliyekuwa amejiuzulu. Ilionekana kuwa hatua hatari kwa sababu De La Fuente alipokezwa mikoba ya Uhispania โ mabingwa mara tatu kutokana na makala matano yaliyopita ya Euro (2008, 2012, 2024) โ bila ya kuwa kocha wa timu kubwa. Baada ya kuangika daluga zake mnamo 1994, De La Fuente alitumia miaka 15 kutekeleza majukumu tofauti katika klabu za ligi za chini za Uhispania akiwa kocha msaidizi kabla ya kuaminiwa fursa ya kunoa makinda wa Uhispania. Mafanikio ya timu za taifa na makocha raia wa Uhispania yameenea hadi katika viwango vya klabu. Licha ya uamuzi wa Pep Guardiola kuondoka Manchester City baada ya miaka 10 ya kuzoa mataji tofauti, angalau robo ya wakufunzi wanaoanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) 2026-27 ni Wahispania.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.