WIRE โ€” Aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Kenya (LSK), Faith Odhiambo, amesema vuguvugu la Linda Mwananchi litageuzwa kuwa chama cha kisiasa kabla ya mwisho wa mwaka huu, huku likijiandaa kushiriki siasa za uchaguzi mkuu wa 2027. Odhiambo alisema maandalizi ya kukisajili chama hicho yanaendelea, ingawa huenda kisitambulike kwa jina la Linda Mwananchi. "Huenda chama kisitumie jina la Linda Mwananchi, lakini tutakizindua mwaka huu," alisema akizungumza katika mahojiano ย na kituo kimoja cha televisheni Jumatatu, Odhiambo, ambaye hivi majuzi alijiunga na vuguvugu hilo linaloongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, alisema hatua hiyo inalenga kupatia kundi hilo jukwaa rasmi la kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Kauli yake inajiri siku chache baada ya viongozi wa Linda Mwananchi kutangaza kuwa wameamua kujiondoa rasmi ndani ya Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), wakisema ni wakati wa kuanzisha mkondo mpya wa kisiasa katika upinzani. Aliyekuwa Mwenyekiti wa LSK Faith Odhiambo . Picha|MaktabaTangazo hilo lilitolewa wakati wa ziara ya viongozi waa vuguvugu hilo katika Kaunti ya Taita Taveta mnamo Julai 18, ambapo walizungumza na wafuasi wao katika maeneo ya Mwatate, Wundanyi na Voi. Akihutubia wafuasi hao, Mbunge wa Suba Kusini na msemaji wa vuguvugu hilo, Caroli Omondi, alisema uhusiano kati ya Linda Mwananchi na ODM umefikia kikomo. "Sasa imefika wakati wa kuvunja uhusiano tuliokuwa nao na Orange Democratic Movement. Ni wakati wa kujiondoa ODM," alisema Omondi. Mbunge huyo pia alikosoa mwelekeo wa sasa wa ODM, akidai kuwa chama hicho kimetema misingi iliyokuwa ikikisimamia. "ODM imesaliti si Raila Odinga pekee, bali pia misingi na maadili aliyokuwa akiyapigania," alisema. Pia alimtaka Rais William Ruto kuruhusu mchakato wa usajili wa chama hicho kuendelea bila kuingiliwa. "Rais Ruto aache kuishinikiza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa kukataa usajili wa chama cha Linda Mwananchi," alisema. Wakati huo huo, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ameendelea kuchochea mjadala wa kisiasa baada ya kudokeza kuwa huenda akawania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Akizungumza katika mkutano huo, Sifuna alisema amepata msukumo kutoka kwa vijana kuwania uongozi wa juu nchini. "Vijana wameniita, na sasa natoka kuwa Katibu Mkuu hadi Ikulu," alisema. Viongozi kadhaa kutoka eneo la Magharibi wanaomuunga mkono Sifuna wamepongeza hatua ya kuanzishwa kwa chama kipya, wakisema kitakuwa chombo muhimu cha kisiasa kitakachowaunganisha wafuasi wake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.