WIRE โ MAKAHAMA ya Juu imeamuru Mwanasheria Mkuu Dorcas Oduor kutoa ushauri kuhusu mtanziko wa kikatiba unaohusu iwapo maafisa wa serikali waliotimuliwa wanaweza kuwania chaguzi huku wakipinga kufurushwa kwao kortini. Korti Ijumaa iliyopita iliagiza Mwanasheria Mkuu kutoa ushauri katika siku 21. Jopo liliwasilisha suala hilo kwa Mwanasheria Mkuu huku likichelewesha uamuzi muhimu ambao huenda ukaathiri chaguzi kuu zijazo za urais 2027. Kesi hiyo ina umuhimu kwa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, aliyekuwa gavana wa Meru, Kawira Mwangaza na aliyekuwa gavana wa Nairobi, Mike Sonko, ambao kung'olewa kwao afisini kumezua makabiliano ya muda mrefu kortini. Kiini cha kesi hiyo ni kuhusu iwapo viongozi waliofurushwa kutoa afisi za umma kupitia mchakato wa sheria wanaweza kuwania afisi za uchaguzi kabla ya kesi zao za rufaa kukamilika. Bw Gachagua alitimuliwa na Bunge la Kitaifa 2024 kabla ya kuwasilisha kesi kortini kupinga uhalali wa kumfurusha. Mvutano huo unaendelea katika Mahakama ya Rufaa. Ni miongoni mwa wapeperushaji bendera wanaodhamiria kupinga kuchaguliwa tena kwa Rais William Ruto, katika uchaguzi mkuu wa Agosti 2027. Bi Mwangaza alitemwa kama gavana wa Meru Agosti 2024 baada ya Seneti kupitisha uamuzi wa bunge la kaunti kumng'atua mamlakani, na kuzua kesi tofauti kortini kuhusu mchakato. Bw Sonko alitimuliwa kama gavana wa Nairobi 2020 na akaendelea kukabiliana kisheria kuhusu ufurushaji wake huku akijihusisha na siasa. Kufuatia kubanduliwa kwao walianzisha vyama tofauti vya kisiasa, huku Bw Gachagua akiwa kinara wa Democracy for the Citizens Party (DCP), Bw Kawira Umoja na Maendeleo Party (UMP) huku Sonko akiongoza National Economic Development Party (NEDP). Kesi iliyo mbele ya Mahakama ya Juu iliwasilishwa na Spika wa Bunge la Kaunti ya Meru, Ayub Bundi Solomon, Aprili 2026 kwa namna ya ushauri wa kurejelewa, akiomba korti hiyo kutafsiri Sura ya Sita ya Katiba pamoja na Vifungu 99 na 193 vinavyosimamia kufuzu na kung'olewa kutoka afisi ya uchaguzi. "Haya ni marejeleo kuhusu ushauri. Marejeleo haya yanatokana na utata ambao haujatatuliwa katika kitovu cha mfumo wa uongozi na uadilifu chini ya Sura ya Sita ya Katiba," anasema. Katika kesi iliyowasilishwa Aprili 10, 2026, Bw Bundi alihoji kuwa amri za korti zinazofutilia mbali ufurushaji zikisubiri rufaa, kimtindo, zimeruhusu maafisa walioondolewa kwa mashtaka ya uadilifu, ikiwemo kutimuliwa, kubaki waliofuzu kwa chaguzi huku kesi zikiendelea. Alifafanua kuwa miaka 15 tangu katiba mpya ilipozinduliwa 2010, "bado hakuna tafsiri thabiti kuhusu ikiwa katiba inabuni kiwango mwafaka kinachoeleweka kuhusu uongozi wa umma hasa kuhusu namna kiwango hicho kinatumika kwa watu waliong'atuliwa afisini." Badala ya kusuluhisha masuala hayo kikatiba papo hapo, jopo la majaji watano wakiongozwa na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu waliagiza Spika Bundi kwanza apate ushauri kisheria kutoka kwa Mwanasheria Mkuu kabla ya kesi hiyo kuendelea kusikizwa. "Mlalamishi ameagizwa kutafuta ushauri wa mwanasheria mkuu, na ushauri huo utolewe katika muda wa siku 21 kuanzia tarehe ya uamuzi huu," iliamuru korti. Majaji wengine wa jopo hilo ni Smokin Wanjala, Isaac Lenaola, William Ouko na Mohamed Warsame. Majaji waliagiza kuwa marejeleo na uamuzi uwasilishwe kwa mwanasheria mkuu na kwamba suala hilo lirejeshwe mbele ya Naibu Msajili baada ya kutimiza masharti hayo. Uamuzi huo vilevile uliahirisha kusikiza ombi lililowasilishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka na Tume ya Maadili ya Kupambana na Ufisadi kujiunga na kesi hiyo. Tume hizo mbili ziliwasilisha ombi kushirikishwa kwa sababu ya majukumu yake kikatiba kuhusu kufuzu kwa mgombea na matakwa ya uadilifu. Spika alihoji kuwa maoni ya Mwanasheria Mkuu kabla ya kuwasilisha marejeleo hayakuwa lazima. Mawakili wake walisisitiza kwamba ushauri tofauti uliotolewa na Korti ya Juu 2024 uliashiria kwamba mchakato si lazima na kwamba muundo wa ugatuzi ulifanya mkondo huo kukosa ustawishaji katika hali hiyo. Majaji walipinga hoja hiyo. "Kanuni 53 ya Sheria za Korti ya Juu 2020, pamoja na orodha ya mamlaka alizonukuu mlalamishi, zinaweka bayana mahitaji ya kutafuta ushauri wa mwanasheria mkuu kabla ya kuwasilisha marejeleo," korti ilisema. Majaji walisema ushauri kama huo, "huenda ukasuluhisha swali lililo mbele yetu kwa namna inayoridhisha mlalamishi, hivyo kuokoa muda muhimu wa korti." Aidha, walihoji kuwa mzozo wa sasa unatofautiana pakubwa na ushauri wa awali kwa sababu mwanasheria mkuu alikuwa mlalamishi katika kesi hiyo na hivyo basi hangetarajiwa kushauri afisi binafsi. Mahakama vilevile ilipuuzilia mbali hoja kuwa mfumo wa ugatuzi unamzuia mwanasheria mkuu kutoa ushauri kuhusu suala hilo. "Mfumo wa ugatuzi jinsi ulivyoundwa kwa sasa haumfungii nje mwanasheria mkuu kutoa ushauri, hasa kwa suala linalohusu umma," majaji walisema. Korti ya juu haikotoa maoni yoyote kuhusu ikiwa maafisa waliong'olewa au kuondolewa mamlakani wanaweza kuwania chaguzi kesi zao za rufaa zikiwa bado hazijakamilika. Badala yake, ilijikita kwenye suala la mchakato lililowasilishwa kwake na kuamuru mwanasheria mkuu kutoa ushauri kwanza kabla ya kikao chochote kuhusu masuala nyeti kikatiba kuendelea. Kesi hiyo imepangiwa kutajwa Agosti
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.