WIRE โ€” CHAMA kipya cha kitaaluma kimezinduliwa nchini ili kuimarisha ulinzi wa haki za kibinadamu za wafanyakazi na jamii zinazoathiriwa kwenye miradi ya kilimo na maendeleo, wasiwasi ukishamiri kuhusu ukiukaji wa haki za wafanyakazi, migogoro ya ardhi na ulegevu wa ulinzi wa kijamii. Social Impact Management Association of Kenya (SIMAK), ni muungano utakaowakutanisha wataalamu wanaohakikisha miradi ya maendeleo, hususan katika kilimo na miundombinu, inazingatia haki za kibinadamu na kushirikisha jamii zinazoathirika. Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Edward Ontita, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi jijini Nairobi alisema lengo ni kuhakikisha kila mradi mkubwa unakuwa na maafisa wa usimamizi wa kijamii kuanzia hatua ya kupanga hadi kukamilika. "Tunataka viwango endelevu vizingatiwe katika miradi yote ya maendeleo. Maendeleo yanawahusu watu, hivyo haki zao lazima zilindwe," akasema. [caption id="attachment_190228" align="aligncenter" width="300"] Kaimu Mwenyekiti wa Social Impact Management Association of Kenya (SIMAK), Profesa Edward Ontita (kulia) akikabidhi mmoja wa wanachama wa muungano huo cheti cha kuwa memba. Picha|Sammy Waweru[/caption] Prof Ontita alisema mashamba makubwa ya kilimo ni miongoni mwa sekta zilizoathirika zaidi na ukatili wa kijinsia, unyanyasaji wa kingono, mishahara duni na mazingira mabaya ya kazi. "Baadhi ya wafanyakazi hulipwa chini ya kiwango cha chini cha mshahara kilichowekwa kisheria, huku wengine wakikosa maji safi, vyoo bora na uhuru wa kujiunga na vyama vya wafanyakazi. Hizi ni haki za msingi za binadamu," alisema. Aliongeza kuwa jamii zinapaswa kushirikishwa kuanzia hatua za kwanza, hasa katika miradi inayohusisha ununuzi wa ardhi na ulipaji wa fidia. Aidha, alisema miradi ya mikopo ya kaboni na uhifadhi wa bioanuwai inapaswa kushirikisha wananchi kikamilifu ili wanufaike. "Kutofuata masharti ya ulinzi wa kijamii husababisha ucheleweshaji wa miradi na hasara ambazo tumefanya hesabu zinafika Sh600 bilioni" Ontita alionya. [caption id="attachment_190230" align="aligncenter" width="300"] Kaimu Mwenyekiti wa Social Impact Management Association of Kenya (SIMAK), Profesa Edward Ontita wakati wa mahojiano jijini Nairobi mnamo Juni 26, 2026. Picha|Sammy Waweru[/caption] Kwa upande wake, Kaimu Karani katika Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Wizara ya Ulinzi wa Jamii na Masuala ya Wazee, Dkt Lynett Ochuma, alisema serikali inaandaa sera ya kitaifa ya kusimamia hatari zinazokumba jamii ili kuoanisha sekta hiyo na viwango vya kimataifa huku ikizingatia mazingira ya wafanyakazi nchini Kenya. Alisema sera hiyo itashughulikia haki za wafanyakazi, afya na usalama wa jamii, kuzuia unyanyasaji wa kingono, kulinda makundi yaliyotengwa na kuhakikisha ununuzi wa ardhi na uhamishaji wa watu unafanyika kwa haki. "Ushirikishwaji wa wadau ni msingi wa maendeleo. Maendeleo hayapaswi kudhuru jamii bali yanapaswa kuwa jumuishi," alisema, akiongeza kuwa sera hiyo itawasilishwa bungeni kama mswada baada ya kukamilika.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.