WIRE โ€” WAFANYAKAZI saba wa shirika la kutoa misaada kutoka Amerika waliokuwa wakisaidia kukabiliana na mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wametengwa kwa siku 21 katika kituo kipya cha uangalizi nchini Kenya, kufuatia masharti mapya ya usafiri yaliyowekwa na serikali ya Amerika. Franklin Graham, rais na mtendaji mkuu wa shirika la misaada la Kikristo la Samaritan's Purse, aliambia Reuters kuwa wafanyakazi hao hawana dalili zozote za Ebola, lakini wanazingatia utaratibu wa kutengwa kama tahadhari. "Wafanyakazi wetu saba wa kundi la Kukabiliana na Majanga wako huko. Hawana dalili zozote, lakini wanatengwa kwa siku 21 chini ya usimamizi wa serikali ya Kenya," alisema Graham. Kwa mujibu wa sera mpya ya Amerika, raia wake wanaorejea kutoka DRC, ambako kuna mlipuko wa Ebola, lazima wakae kwa wiki tatu katika nchi ya tatu kabla ya kuruhusiwa kuingia Amerika. Serikali ya Amerika inajenga kituo chenye uwezo wa vitanda 50 katika kambi ya jeshi la anga katikati mwa Kenya kwa ajili ya kuwafuatilia raia wake ambao huenda waliathiriwa na virusi vya Ebola nchini DRC au Uganda lakini hawajaonyesha dalili za ugonjwa. Ujenzi wa kituo hicho umekumbana na upinzani mkubwa nchini Kenya. Wakenya wengi wanahisi kuwa Amerika inahamishia hatari ya kiafya nchini humo. Mwezi uliopita, Waziri wa Afya alitangaza kusitishwa mara moja kwa ujenzi huo baada ya kupatikana na hatia ya kuidharau mahakama kwa kutotekeleza amri ya kusimamisha shughuli hizo hadi kesi iamuliwe. Afisa wa Wizara ya Masuala ya Kigenu ya Amerika alisema kundi hilo la wahudumu lilihamishiwa kwa hiari katika kituo hicho kwa uangalizi na kutengwa kama tahadhari. Alisema maafisa wa Kenya wameruhusu hatua hiyo chini ya usimamizi wa madaktari wa Huduma ya Afya ya Umma ya Amerika. Chanzo kilichofahamu suala hilo kilisema kundi hilo liliwasili katika kituo hicho Jumatatu. Baadhi yao walikuwa wamewahudumia wagonjwa wa Ebola nchini Congo huku wengine wakifanya kazi za ujenzi bila kukutangamana moja kwa moja na wagonjwa. Kilisema kuna mtu mmoja anayeshukiwa kuwa katika hatari kubwa ya maambukizi, lakini afya ya wote inaendelea kufuatiliwa. Pia maafisa wa Kenya hawajawaruhusu kutoka katika kituo hicho hadi kipindi cha uangalizi kitakapokamilika. Ebola huenea kupitia kugusana moja kwa moja na majimaji ya mwili ya mtu au mnyama aliyeambukizwa. Shirika la Samaritan's Purse ni miongoni mwa mashirika makubwa yanayosaidia kukabiliana na Ebola nchini DRC kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO). Aina ya virusi vya Bundibugyo, ambayo haina chanjo wala tiba iliyothibitishwa, imeua angalau watu 828 tangu katikati ya Mei. WHO inasema maambukizi bado yanaendelea kusambaa bila kutambuliwa kwa kiwango kikubwa. Graham alisema baada ya kutembelea kituo hicho wiki hii ameridhishwa na vifaa vilivyopo. "Ni kituo cha kisasa kabisa. Iwapo mtu angeugua, hapo ndipo mahali pazuri pa kumpatia matibabu," alisema.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.