WIRE โ€” WAAMERIKA saba wa shirika la misaada wanaougua Ebola wamewekwa kwenye kituo cha karantini nchini Kenya, ripoti iliyochapishwa kwenye shirika la habari la kimataifa Reuters imeonyesha. Kulingana na ripoti hiyo, afisa mkuu wa shirika la Samaritan's Purse Franklin Graham ananukuliwa akithibitisha habari hizo akisema hatua hiyo imetokana na vikwazo vya kiusafiri vilivyowekwa na utawala wa Rais Donald Trump kuhusu raia walioambukizwa wanaorejea nyumbani. Habari hizi zinaweza kugutusha Wakenya wengi ambao wamekuwa wakipinga kuanzishwa kwa kituo cha karantini ya Ebola nchini kwa misingi kwamba hatua hiyo italeta ugonjwa huo hatari katika ardhi ya Kenya ambayo haijawahi kuthibitisha kuweko kwa maradhi hayo, na pia kwamba mifumo ya afya huenda isiwe thabiti kiasi cha kuweza kupambana na msambao wa maradhi hayo. Kumekuwa pia na kesi mahakamani ambapo Waziri wa Afya Aden Duale aliitwa kuthibitisha kwamba ujenzi wa kituo cha karantini uliokuwa umeanzishwa katika kambi ya kijeshi ya Nanyuki, Laikipia umethibitishwa. Bw Duale alikuwa ameshutumiwa na korti kwa kupuuza maagizo ya kusitisha ujenzi huo hadi kesi iliyowasilishwa na kupinga ujenzi huo kusikizwa na kuamuliwa. Mahakama ilikuwa tayari kutoa adhabu kwa Bw Duale ila ikabadili nia pale waziri alipowasilisha stakabadhi kuthibitishia mahakama kwamba imetekeleza maagizo ya kusitisha ujenzi wa karantini hiyo. Awali, utawala wa Rais Trump kupitia ripoti mbali mbali ulikuwa umesisitiza kwamba utaheshimu maamuzi ya korti ya kutojenga kituo cha karantini na kutuma raia wake wanaougua nchini Kenya. Hata hivyo, Rais William Ruto amekuwa akitetea ujenzi wa kituo cha Laikipia, akisema hicho kilikuwa kimoja kati ya vituo vingine vilivyokuwa vinajengwa nchini na kwamba Kenya ina jukumu la kuwa rafiki mwema wa kusaidia raia wa Amerika walioambukizwa, akisema pia ujenzi wenyewe ulikuwa unafanywa kwa pesa za Amerika.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.