WIRE โ€” KIKAO cha kundi la wabunge kilichojawa na vurugu usiku wa manane Jumatano kilisababisha pigo jingine kwa Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna. Baada ya kikao hicho, jana katibu huyo wa zamani wa ODM alitimuliwa katika wadhifa wake wa Kiranja wa Wachache huku migawanyiko ikichacha katika upinzani. Mkutano huo uliofanyika katika afisi ya Kiranja wa Wachache wa Bunge la Seneti, Ledama ole Kina ulifichua migawanyiko katika muungano wa Azimio na kuzidisha madai kwamba kundi la maseneta wa ODM lilitekeleza mpango uliodaiwa kupangwa awali mapema katika kikao na Rais William Ruto katika ikulu. Spika wa Seneti, Amason Kingi tayari ametekeleza mabadiliko. Seneta wa Migori Eddy Gicheru Oketch amechukua usukani wa afisi hiyo. Uamuzi huo ulijiri siku chache tu baada ya Bw Sifuna kupoteza wadhifa mwingine muhimu alipotemwa kutoka kwa kamati maarufu ya kawi ya seneti inayoongozwa na kinara wa ODM Oburu Oginga. Hatua hiyo vilevile ilifuatia kung'olewa kwake kama Katibu Mkuu wa ODM, uamuzi alioapa kupinga, kuashiria kampeni kali ya kambi hiyo inayounga mkono serikali ya muungano kudidimiza ushawishi wake. Mkutano wa Jumatano ulijawa na sarakasi tele huku ukigeuka upesi mapambano ya kimchakato yaliyoishia kuwa majibizano makali na makabiliano miongoni mwa maseneta kuhusu uhalali wa kikao hicho. Kundi la maseneta waliozungumza na Taifa Leo walidai waligutuka kupokea notisi kuhusu kikao hicho saa chache tu kabla ya kuanza. Notisi hiyo iliyotumwa na Kiongozi wa Wachace katika Seneti, Ole Kina mwendo wa saa kumi na mbili kasorobo iliwaalika maseneta kuhudhuria kikao cha kundi la wabunge mwendo saa moja unusu usiku afisini mwake. Mawasiliano hayo hayakueleza ajenda, jambo lililozua shaka miongoni mwa maseneta wanaoegemea upande wa Bw Sifuna na kundi la kujitenga la Linda Mwananchi, wengi wao waliosikia ripoti kuwa kundi la maseneta wa ODM walikuwa ikulu adhuhuri. Kulingana na waliohojiwa, wasiwasi uliongezeka kwa sababu mwaliko ulijiri saa chache baada ya wajumbe wa ODM wakiongozwa na Dkt Oginga kushiriki chamcha kilichoandaliwa na Rais Ruto katika ikulu. Seneta wa Kisumu, Tom Ojienda alithibitisha kuwa baadhi ya maseneta walihudhuria hafla hiyo. "Tulienda kushiriki chamcha na Rais, jambo ambalo ni la kawaida. Ni kawaida kwetu kushiriki maakuli ya mchana na Rais kwa hivyo haihusiani na hatua hii," akasema Seneta Ojienda. Alithibitisha vilevile kuwa yeye binafsi aliwasilisha hoja ya kumtimua Sifuna. "Ni mimi niliwasilisha hoja ya kumwondoa Sifuna," alisema. Wanachama waliuliza kwa nini kikao kiliandaliwa kupitia notisi fupi jinsi hiyo na kwa nini maseneta hawakufahamishwa mbeleni kwamba mabadiliko ya uongozi yalikuwa sehemu ya ajenda. Wengine walihoji kuwa uamuzi muhimu jinsi hiyo haungefanywa haraka bila kuwapa wanachama wote wa muungano muda wa kutosha kuhudhuria.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.