WIRE โ€” KILA siku mayai zaidi ya 2,500 huwekwa kwenye kitotoa, mamia ya vifaranga wanaanguliwa kila baada ya siku 21, huku wafanyakazi wakikesha kuhakikisha zaidi ya kuku 150,000 wa kienyeji wanapata chakula, maji na uangalizi unaohitajika. Hivi ndivyo Nick Mwendwa, aliyewahi kuongoza Shirikisho la Soka Kenya (FKF), anavyosimamia moja ya mashamba makubwa zaidi ya kuku halisi wa kienyeji nchini katika eneo la Kalii mjini Makindu, Kaunti ya Makueni. Kilichoanza miaka mitatu iliyopita kwa kuku saba waliokuwa wa mamake, sasa kimegeuka kuwa mradi mkubwa wa ufugaji unaotegemea teknolojia ya kisasa. Safari hii ya kuwekeza katika kuku wa kienyeji haijakuwa rahisi. "Sikuwa na ujuzi wowote wa ufugaji kuku. Nilikumbwa na changamoto si haba ikiwemo kiwango duni cha kuanguliwa kwa mayai, gharama kubwa ya lishe, na kupotea kwa umeme kila mara ambako kulitishia uzalishaji," Mwendwa anaambia Akili Mali tulipotembelea mradi huo. [caption id="attachment_190105" align="alignnone" width="2560"] Rais wa zamani wa FKF Nick Mwendwa akiokota mayai shambani mwake Makueni. Picha|Evans Habil[/caption] Changamoto kuu ambayo nusra izime ndoto yake ni kupoteza vifaranga wapatao 500 kutokana na sababu ya kukosa ufahamu wa jinsi ya kuchanganya chakula chao. Mwendwa anasema wazo la kuingilia ufugaji halikutokana na mapenzi ya kilimo, bali baada ya kushindwa kupata kuku halisi wa kienyeji katika maduka makubwa. "Niligundua mahitaji yalikuwa makubwa kuliko uzalishaji. Wakulima wengi walikuwa wamehamia kufuga aina ya kuku walioboreshwa (layers na broilers), lakini walaji bado wanataka ladha ya kuku halisi wa kienyeji," anasema. Baada ya kufanya utafiti katika masoko ya Ukambani, alibaini kuwa madalali walikuwa wakinunua kila kuku wa kienyeji aliyeletwa sokoni na kuwapeleka Nairobi, jambo lililodhihirisha gapu kubwa ya biashara hiyo. Hapo ndipo alipoanza mradi wake kwa kuku saba waliokuwa wa mamake. "Niliwatenga na kuamua kizazi chote kitokane na hao pekee ili kuhifadhi uhalisia wa mbegu," anaelezea. Mwanzoni, hata wazazi wake hawakuamini ndoto yake. "Mamangu alicheka niliposema nataka kufikisha kuku 15,000. Baadaye nilipoweka lengo la kuku milioni moja, baba alisema Nairobi imenichanganya," akaambia 'Akilimali' shambani mwaki eneo la Kalii, Makindu huku akitabasamu. Changamoto nyingine ilianza baada ya mayai karibu 450 kushindwa kuanguliwa, hali iliyomlazimu kununua mashine ya kwanza ya kuatamia mayai. [caption id="attachment_190106" align="alignnone" width="2560"] Mwendwa akionyesha mayai yaliyotagwa katika shamba lake la kuku Makueni. Picha|Evans Habil[/caption] Matokeo ya awali hayakuridhisha kwani ni asilimia 41 pekee ya mayai yaliyoanguliwa. Badala ya kukata tamaa, alianza kufanya utafiti na kutumia Akili Unde (AI) kuchambua mashine zake. Baada ya kurekebisha mfumo wa hewa na mpangilio wa trei, kiwango cha uanguaji kiliongezeka hadi asilimia 81. Teknolojia pia ilinisaidia kupunguza gharama za uzalishaji, Mwendwa akasema. Alianzisha kiwanda chake cha kutengeneza chakula cha kuku kwa kutumia mahindi, soya na malighafi nyinginezo zenye virutubisho, hatua ambayo anasema imepunguza gharama za malisho kwa zaidi ya asilimia 60. Hali kadhalika, Rais huyu wa zamani wa FKF analima Azolla, mmea wa majini ya kijani wenye protini nyingi unaotumika kulisha kuku. Baada ya kukumbwa na kisa cha kukatika kwa nguvu umeme kwa saa nane, aliwekeza katika mfumo wa nishati ya jua ili kuhakikisha mashine za kuatamia zinaendelea kufanya kazi bila kusimama. Licha ya kuwa na zaidi ya kuku 150,000 kwa sasa, Mwendwa bado hajaanza kuuza kwa kiwango kikubwa. "Ninalenga kufikisha kuku 400,000 kufikia Desemba mwaka huu wa 2026 kabla ya kuingia kikamilifu sokoni ili niweze kukidhi mahitaji ya maduka makubwa na wateja wengine," anadokeza. Anachofanya kwa sasa ni kuuza jogoo moja moja. Mradi wake sasa umeajiri wafanyakazi 54 wa kudumu huku Mwendwa akisisitiza kuwa mafanikio yake yametokana na uvumilivu na utatuzi wa changamoto moja baada ya nyingine.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.