WIRE โ NI mwamko mpya kwa wakulima wa miwa katika Kaunti ya Bungoma, baada ya kampuni ya kutengeneza sukari ya Nzoia kuripoti kuwa imelipa wakuzaji zaidi ya Sh700 milioni tangu irejelee shughuli zake mwaka huu. Katika taarifa wiki jana Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) Sohan Sharma alisema kampuni hiyo pia imeripoti kuimarika kwa uzalishaji na uwekezaji katika mchakato wa utengenezaji bidhaa zinginezo. "Kwa sasa wakulima wanapokea malipo wiki mbili baada ya kuwasilisha miwa yao kiwandani. Kufikia sasa tumetoa Sh760 milioni kama malipo," akaeleza Sharma. Wakati huo huo, afisa mkuu huyo alisema Nzoia Sugar ilianzisha mpango wa kuboresha mitambo yake baada ya kuwekwa chini ya urasimu wa mwekezaji wa kibinafsi mnamo Mei 2025. "Kampuni ya sukari ya Nzoia ilirejelea shughuli za utengenezaji sukari mnamo Januari 2026 na tangu wakati huo imesaga tani 292, 980 za miwa," Sharma akaongeza.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.