WIRE โ NAIBU wa Rais Prof Kithure Kindiki yuko pazuri kudumisha nafasi yake kama mgombea-mwenza wa Rais William Ruto, kulingana na matokeo ya utafiti. Kwa mujibu wa matokeo ya Infotrak, Prof Kindiki amewazidi kwa mbali wanasiasa wengine ndani ya Serikali Jumuishi. Hapo jana, utafiti huo ulionyesha kuwa Prof Kindiki anaongoza kwa asilimia 34 kati ya wale wanaotajwa kuwa wagombea-wenza wa Rais Ruto na ni pekee aliyepata zaidi ya asilimia 20. Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga anafuata kwa asilimia 11, huku Kiongozi wa ODM, Dkt Oburu Oginga na Waziri wa Madini Hassan Joho wakiwa na asilimia tano na nne mtawalia. Bi Wanga ashatangaza kuwa analenga kutetea kiti chake Homa Bay naye Dkt Oginga analenga Useneta wa Siaya kwa mara nyingine. Bw Joho amekuwa akisukumwa na baadhi ya wanasiasa kutoka ukanda wa Pwani ambako ana ushawishi mkubwa wa kisiasa. Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya, Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangรบla na Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi wamekuwa wakitajwa na baadhi ya wanasiasa kutoka Magharibi mwa nchi kama wanaotea nafasi ya Profesa Kindiki lakini hawakuorodheshwa popote. Wiki jana, Bw Mudavadi hata hivyo akiwa Kaunti ya Trans Nzoia, aliweka wazi kuwa hataki kuwa mgombeaji mwenza wa Rais Ruto bali analenga kuwahi urais mnamo 2032. Kinaya ni kuwa eneo la Magharibi na Nyanza, Prof Kindiki anapigiwa upatu kwa asilimia 36 and asilimia 28. Kiwango cha Nyanza kinazidi hata asilimia 21 ya Bi Wanga eneo hilo. Vivyo hivyo Pwani mwa nchi, Bw Joho ana asilimia 11 huku Profesa Kindiki akiwa na asilimia 23. Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku amekuwa akiongoza viongozi wa Mlima Kenya Mashariki kusisitiza kuwa Prof Kindiki asalie naibu rais huku akisema wako tayari kuagana na wenzao wa Mlima Kenya Magharibi debeni kama hawataungwa mkono. Katika eneo la Mlima Kenya, Profesa Kindiki alijizolea asilimia 22 kati ya wale ambao wanataka awe mgombeaji mwenza wa Rais. Katika matokeo ya utafiti wa TIFA yaliyotolewa mnamo Mei 14, Profesa Kindiki alikuwa na asilimia 59 huku Bi Wanga aliyemfuata akiwa na asilimia 12. Dkt Oginga alipata asilimia tatu huku Bw Joho akitoka na asilimia moja. Iwapo matokeo haya ni ya kuzingatiwa, basi huenda mjadala wa nani anastahili kuwa mgombeaji mwenza wa Rais 2027 ukatatuliwa mapema na kumwezesha kujipanga. Kama mwishowe Rais atamteua Profesa Kindiki kama mgombeaji mwenza ana nafasi ya kuwahi zaidi ya kura 1.3 za Mlima Kenya Mashariki ambazo ni kaunti za Embu, Meru na Tharaka-Nithi
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.