WIRE โ€” TEHRAN, Iran: MASHAMBULIZI baina ya wanajeshi wa Amerika na Iran yaliyoendelea tokea wikendi yamechangia kupanda tena kwa bei ya mafuta ulimwenguni. Iran ililenga vituo vya kijeshi vya Amerika katika eneo la Ghuba na kutangaza kuwa imefunga tena Mlango-bahari wa Hormuz. Wanajeshi wa Iran Jumatatu walisema walilenga kambi za jeshi la Amerika nchini Bahrain na Kuwait na kuharibu vifaa vya kijeshi nchini Oman. Pia Iran ilishambulia ghala la silaha katika kambi ya jeshi la Anga la Prince Hassan nchini Jordan huku ikilipiza kisasi shambulizi lolote linalotekelezwa na Amerika. Amerika nayo ilishambulia mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran, kambi ya jeshi pwani na boti za kijeshi. Ilitumia ndege za kivita, meli za kijeshi na ndege zisizo na rubani (droni). Mapigano hayo yanaonyesha kuwa muafaka wa kusitisha vita kati ya nchi hizo mbili sasa umekiukwa. Muafaka huo uliafikiwa mnamo Juni na ulilenga kufungua Mlango-bahari wa Hormuz na kusitisha vita kabisa kwa siku 60. Katika mahojiano mafupi na Reuters Jumapili, Rais wa Amerika Donald Trump alitabiri kuwa mara hii watalemea Iran katika vita hivyo. "Tunawashinda vibaya," akasema Trump. Kiongozi huyo tayari ameweka wazi kuwa hatilii manani muafaka uliotiwa saini ambao anasema umekufa japo akasema iwapo Iran inataka kunusurika bado kutakuwa na mazungumzo. Mwakilishi wa Iran kwenye mazungumzo na Amerika, Mohammad Baqer Qalibaf amesema kuwa wapo tayari kwa vita na hawatakubali kuhadaiwa tena. "Enzi za makubaliano yanayoegemea upande mmoja zimekwisha. Tuliwaambia watimize ahadi zeo au walipe gharama na sasa ukweli unaonekana," akasema. Vita vilivyoanzishwa na Amerika-Israel dhidi ya Iran mnamo Februari 28 vimevuruga usalama katika eneo la Ghuba na kuenea katika Mashariki ya Kati. Iran imeonyesha uwezo mkubwa wa kijeshi na umekuwa ukishambulia kambi za wanajeshi wa Amerika Mashariki ya Kati. Vita hivyo vimesababisha maelfu ya watu kuuawa, wengi wao wakiwa Iran na Lebanon. Iran imezima shughuli katika Strait of Hormuz na sasa kando na bei ya mafuta kupanda kuna mfumuko wa bei ya bidhaa kote ulimwenguni. Aidha Iran inasisitiza kuwa itafungua mkondo huo na kuruhusu meli za kupitisha mafuta iwapo Amerika itazima shughuli za kijeshi katika Pwani yake.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.