WIRE — WIZARA ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo inaendelea na mazungumzo na Wizara ya Fedha na Hazina ya Kitaifa ili kuondoa ushuru (VAT) kwenye mitambo ya uchakataji na uongezaji thamani wa mazao ya kilimo, hatua inayolenga kusaidia ukumbatiaji matumizi ya teknolojia, kuongeza uzalishaji na kuboresha ushindani wa bidhaa za Kenya katika soko la kimataifa. [caption id="attachment_190047" align="aligncenter" width="300"] Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe akiendesha trekta aina ya Sonalika wakati wa uzinduzi wake KICC, Nairobi na Elgon Kenya. Picha|Sammy Waweru[/caption] , anasema pendekezo hilo linahusu mitambo inayotumika kuchakata maziwa, chai na mazao mengine ya kilimo. Anasema kupunguza gharama ya kununua vifaa hivyo kutaboresha uwekezaji katika mtandao mzima wa thamani wa sekta ya kilimo. Akizungumza jijini Nairobi majuzi katika hafla ya kampuni ya Elgon Kenya kuzindua usambazaji wa trekta za Sonalika, ukumbi wa KICC, Kagwe alisema matumizi ya teknolojia ya kisasa ni nguzo muhimu katika mpango wa serikali wa kubadilisha kilimo kuwa biashara ya kisasa, yenye faida na inayovutia vijana. "Mbali na matrekta, tunataka pia vifaa vya uchakataji na uongezaji thamani wa mazao viondolewe VAT. Hatua hii itaimarisha biashara ya kilimo, kuongeza ushindani wa bidhaa zetu na kukuza mauzo ya mazao nje ya nchi," alisema. Waziri alibainisha kuwa matrekta tayari hayatozwi ushuru, jambo lililosaidia kupunguza gharama za kuyapata. Kuondoa VAT kwenye mitambo ya uchakataji kutachochea uwekezaji na ukuaji wa viwanda vijijini. Kagwe alisema changamoto kubwa zinazokwamisha matumizi ya teknolojia ni gharama kubwa za mitambo na baadhi ya wakulima kung'ang'ania mbinu za zamani za uzalishaji. "Ndio maana ushiriki wa vijana ni muhimu. Wako tayari kukumbatia teknolojia mpya na mbinu za kisasa za kilimo," alisema. [caption id="attachment_190048" align="aligncenter" width="300"] Dkt Bimal Kantaria, Mkurugenzi Mkuu Elgon Kenya akitazama trekta la Sonalika. Picha|Sammy Waweru[/caption] Kagwe aliongeza kuwa matumizi ya teknolojia na mifumo ya kidijitali yatavutia vijana wanaotazama kilimo kama biashara badala ya shughuli ya kujikimu. Kwa miaka mingi, matrekta mengi yamekuwa yakiuzwa kwa zaidi ya Sh4 milioni, hali inayofanya wakulima wengi kushindwa kuyamudu. Hata hivyo, Kagwe alisema matrekta ya Sonalika yanayouzwa kwa bei ya kuanzia karibu Sh1.4 milioni yataongeza upatikanaji wa teknolojia hiyo kwa wakulima, vyama vya ushirika na biashara za vijijini. Mkurugenzi Mkuu wa Elgon Kenya na Mwenyekiti wa Agriculture Sector Network (ASNET), Dkt Bimal Kantaria, alisema kampuni hiyo inalenga kuwapa wakulima wadogo matrekta bora kwa gharama nafuu. "Sonalika ina zaidi ya matrekta milioni moja yanayotumika duniani, huku India ikizalisha karibu milioni moja kila mwaka," Dkt Kantaria alielezea. Alisema Elgon Kenya imeshirikiana na benki za Equity, Stanbic na Prime kutoa mikopo ya hadi asilimia 90 kununua trekta, hivyo mkulima anaweza kulinunua akiwa na kima cha Sh200,000 huku pesa zilizosalia akilipa mashirika hayo ya kifedha polepole. Aidha, Elgon Kenya inapanga kuanzisha matumizi ya droni na suluhu za kilimo zinazotumia akili bandia (AI), ili wakulima waweze kupata huduma za kisasa kupitia simu za mkononi.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.