WIRE โ€” MWANASHERIA mkuu na Waziri wa Fedha, John Mbadi wameitaka Mahakama Kuu kusimamisha kusikizwa kwa kesi muhimu inayohusu uhalali wa deni la umma la Sh7 trilioni inayosubiri rufaa. Wanahoji kuwa korti iliruhusu kwa njia isiyofaa kesi hiyo kusonga mbele licha ya uchunguzi maalum unaoendelea, wakisema kesi hiyo ipo chini ya jukumu la mkaguzi mkuu wa fedha za serikali kikatiba kabla ya korti kuingilia kati. Ombi hilo limetokana na uamuzi uliotolewa Juni 25, 2026 na majaji Justices Francis Gikonyo, Roselyne Aburili na Moses Ado, waliotupilia mbali hoja ya mwanasheria mkuu kwamba kesi hiyo, ambayo vilevile inaitisha ufichuzi wa deni la umma, ilikaidi kanuni za kukamilisha njia zote, ukomavu na kutenganisha mamlaka. Mwanasheria mkuu Dorcas Oduor na Bw Mbadi wanaazimia kusimamisha kikao cha kusikiza kesi hiyo kilichopangiwa kufanyika Oktoba, wakionya kwamba michakato ya kesi itahujumu rufaa inayodhamiriwa na kuvuruga mchakato wa uangalizi kikatiba. Mwanasheria Mkuu hajaridhishwa na uamuzi wa mahakama uliopuuzilia mbali jaribio lake la kusimamisha kesi ili kuruhusu uchunguzi maalum unaofanywa na mkaguzi mkuu, hivyo kusababisha rufaa hiyo inayopangiwa kuwasilishwa. "Baada ya kukosa kuridhishwa na uamuzi mwanasheria mkuu aliwasilisha notisi ya kukata rufaa Juni 30, 2026 akieleza nia ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wote. Iwapo kesi kuhusu suala hili haitasimamishwa, rufaa inayokusudiwa itaishia kuwa kazi bure," anahoji wakili wa serikali Samwel Kaumba, akimwakilisha mwanasheria mkuu katika nakala za korti. Kesi iliyowasilishwa na Seneta wa Busia, Okiya Omtatah na walalamishi wengine wanane, inapinga ufaafu kikatiba wa takriban Sh6.95 trilioni za ukopaji wa umma zilizolundikana kati ya miaka ya fedha 2014/15 na 2023/24 ikiwemo mikopo ya Eurobond. Aidha, inaitisha kutangazwa kwa uhalali kuhusu mchakato wa ukopaji, uwajibikaji wa maafisa wa umma na uhalali kikatiba wa visehemu vya Sheria kuhusu Usimamizi wa Fedha za Umma. Walalamishi vilevile wanataka uamuzi kuhusu iwapo maafisa wa umma wa zamani na wa sasa, ikiwemo wanaoshikilia afisi za Hazina Kuu, Mdhibiti Bajeti na Mkaguzi Mkuu wanapaswa kuwajibika binafsi chini ya Kifungu 226(5) cha Katiba kuhusu madai ya kuelekeza, kuidhinisha au kuruhusu vitendo vinavyodaiwa kuwa haramu vya ukopaji, utowaji fedha, matumizi ya malipo ya fedha za umma kinyume cha sheria. Katika kesi mpya iliyowasilishwa, mwanasheria mkuu anasema korti inapaswa kusimamisha kesi zote hadi Korti ya Rufaa itakapotoa uamuzi kuhusu rufaa inayonuiwa kuwasilishwa.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.