WIRE โ€” Timu ya Kenya ya vichuna chini ya miaka 17, Junior Starlets, imefuzu Kombe la Dunia la Mwaka huu,ย ย baada ya kuichabanga Afrika Kusini 3-1 katika mechi ya marudiano ya hatua ya mwisho jana ugani Nyayo.ย  Kenya ilifuzu kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya pia kushinda mechi ya kwanza 2-0 mjini Pretoria wiki iliyopita. Ushindi huo umeihakikishia Kenya tiketi ya kushiriki fainali zitakazoandaliwa nchini Morocco kuanzia Oktoba 17 hadi Novemba 8, 2026. Hii ni mara ya pili kwa Junior Starlets kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia baada ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika makala ya 2024 yaliyofanyika nchini Jamhuri ya Dominika chini ya ukufunzi wa Mildred Cheche. [caption id="attachment_190028" align="alignnone" width="1296"] Wachezaji wa Junior Starlets wakisherehekea baada ya kufunga bao dhidi ya Afrika Kusini na kufuzu Kombe la Dunia la wachezaji chini ya miaka 17 katika uga wa Nyayo jijini Nairobi jana. PICHA |HISANI[/caption] Mechi hiyo ilianza kwa dakika moja ya ukimya kumuenzi mchezaji wa zamani wa timu ya taifaย ย ya Afrika Kusini, Jayden Adams, aliyefariki dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 25. Kocha Cheche alianzisha kikosi kilekile kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-0 mjini Pretoria. Mishel Ng'ono alianza langoni huku safu ya ulinzi ikiongozwa na Brendah Awuor, Fleviah Khatenje, Sylvia Namisi na Berveline Awuor. Kiungo kilikuwa na Noelina Akuku, Mwanakombo Bakari na Gaudencia Maloba huku Lindey Weey Atieno na Faith Boke wakimsaidia mshambuliaji Brenda Achieng. Afrika Kusini ilianza kwa kasi na kupata bao la mapema katika dakika ya tano kupitia kwa nahodha Katleho Malebana baada ya safu ya ulinzi ya Kenya kufanya makosa. Dakika tatu baadaye, Kenya ilikaribia kusawazisha baada ya Faith Boke kumpasia Brenda Achieng aliyebaki ana kwa ana na kipa, lakini shuti lake halikulenga lango. Kenya iliendelea kushinikiza na kupata mpira wa adhabu katika dakika ya 15 baada ya Achieng kuchezewa visivyo nje ya eneo la hatari, lakini mpira wa Lindey Weey ulipaa nje. [caption id="attachment_190027" align="alignnone" width="2560"] Kiungo wa Junior Starlets Gaudencia Maloba akisherehekea baada ya kufunga bao dhidi ya Afrika Kusini katika uga wa Nyayo jijini Nairobi jana. PICHA |HISANI[/caption] Afrika Kusini ilipoteza nafasi nzuri ya kuongeza bao katika dakika ya 18 wakati Pilate Moloi alipompita kipa Ng'ono na mabeki wawili kabla ya shuti lake kupita nje kidogo ya lango. Licha ya Kenya kutawala mchezo katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, ilishindwa kutumia vyema nafasi ilizopata na kwenda mapumzikoni ikiwa nyuma 1-0. Mwanzoni mwa kipindi cha pili, Cheche alimleta Emily Adhiambo kuchukua nafasi ya Lindey Weey, mabadiliko yaliyoongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Kenya. Starlets waliendelea kulisakama lango la wageni huku Achieng akikaribia kusawazisha katika dakika ya 54, lakini shuti lake liligonga wavu. Shinikizo la Kenya lilizaa matunda dakika ya 70 wakati Gaudencia Maloba aliposawazisha. Kenya iliongeza bao la pili kupitia kwa Awuor aliyefunga kwa mkwaju wa penalti baada ya wenyeji kutunukiwa adhabu hiyo. Mshambuliaji wa akiba Elizabeth Alizeba Achieng alihitimisha ushindi huo katika dakika za nyongeza kwa kufunga bao la tatu na kuiwezesha Kenya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kufuzu kwa jumla ya mabao 5-1. Sasa Junior Starlets wataelekeza macho yao nchini Morocco wakilenga kufanya vizuri zaidi kuliko walivyofanya katika ushiriki wao wa kwanza wa Kombe la Dunia mwaka 2024

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.