WIRE โ KAMPUNI ya stima Kenya (KPLC) imekanusha madai kuwa iliondoa transfoma 15 kutoka maeneo mbalimbali katika eneo bunge la Mbeere North, Kaunti ya Embu, kwa sababu za kisiasa, ikisema vifaa hivyo vilichukuliwa kwa ukarabati wa kawaida. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Meneja wa KPLC Kaunti ya Embu, Bw Vincent Okello, alisema transfoma zinapopata hitilafu kama kuingia maji au kasoro nyingine ambazo haziwezi kurekebishwa zikiwa eneo la matumizi, hupelekwa kwenye karakana maalumu kwa ukarabati, majaribio na kukaushwa kwa teknolojia maalumu ili kurejesha ubora wake. Alisema kati ya Mei na Juni mwaka huu, transfoma 15 ziliondolewa Mbeere North kutengenezwa. Kati ya hizo, 14 tayari zimerejeshwa na kufungwa upya, huku moja iliyoharibiwa na wahuni wiki iliyopita ikibadilishwa Ijumaa. "Kazi hizi ni za kiufundi pekee na zinalenga kuhakikisha wananchi wanapata umeme salama, wa kutegemewa na ulio thabiti," alisema Bw Okello. Hata hivyo, wakazi walipinga madai kwamba walihusishwa kabla ya transfoma hizo kuondolewa. Walisema walishtushwa na hatua hiyo na kudai baadhi ya transfoma zilirejeshwa usiku baada ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu kero hiyo.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.