WIRE โ€” WASHINGTON, Amerika: JESHI la Amerika limesema lilianzisha uvamizi dhidi ya Iran ili kuhakikisha Mkondo-bahari wa Hormuz unafunguliwa kwa usafirishaji wa mafuta na bidhaa nyingine muhimu duniani. Hatua hiyo imesababisha Iran nayo kulipiza kisasi kwa kushambulia kambi za kijeshi za Amerika nchini Kuwait na Bahrain. Vita kati ya mataifa hayo mawili vimechipuka upya huku mazungumzo ya kusitisha vita kati yao yakionekana kutozaa matunda yoyote hivi karibuni. Amerika ilishambulia Iran baada ya nchi hiyo kushambulia meli za kusafirisha mizigo. Rais wa Amerika, Donald Trump tayari amesema kuwa mazungumzo ya kusaka amani na Iran yamekufa na sasa ni wakati wa kurejelea vita. "Wanajeshi wa Amerika wameanza kuendeleza mashambulizi zaidi dhidi ya Iran ili kuwalemaza wasiwe na nguvu tena ya kuzuia usafirishaji wa mafuta na mali kwenye Mlango-bahari wa Hormuz," akasema Kamanda wa jeshi la Amerika katika Ukanda wa Mashariki maarufu kama CENTOM kupitia X. "Amerika inalaumu Iran kwa kushambulia meli ambazo zilikuwa zikipitia mkondo wa Hormuz na kuhatarisha maisha ya manahodha wake," ikaongeza. Mashambulizi ya Amerika yalivuruga miji mingi Kusini mwa Pwani ya Iran huku baadhi ikikosa umeme. Iran nayo ilijibu kwa kushambulia Kuwait na Bahrain ambazo zina makao ya wanajeshi wa Amerika. Wizara ya Ulinzi ya Kuwait ilisema kuwa ilikuwa ikitungua droni na makombora kutoka Iran lakini Qatar nayo ilitoa onyo la kiusalama. Afisa mmoja wa usalama wa Amerika alisema kuwa mashambulizi dhidi ya Iran yataongezeka na kuonya kuwa mara hii wanalenga kulemaza taifa hilo kabisa kijeshi.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.