WIRE โ WAFUASI wake wanamuita 'Comando' jina la utani kuashiria kuwa ni mpambanaji. Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya anajulikana kwa jina hilo. Ni mwanzilishi wa vuguvugu la "Tawe Movement" ambalo chimbuko lake ni kabila la waluhya kusema kukataa. Akianzisha kauli mbiu hiyo alisema kuwa jamii ya waluhya imekuwa nyuma katika uwakilishi serikalini na maeneo muhimu. Amepiga kelele kuanzia mwaka 2023 na kushika kasi zaidi miaka iliyofuatia hadi wakati huu. Sasa, Natembeya ana kazi kubwa kuuza sera ya seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuwa Rais wa Kenya lakini kuu zaidi ni kuhakikisha kuwa ana mbawa nyumbani โ yaani kwa jamii ya Mulembe. Katika mazishi ya kakake mbunge wa Bumula Jack Wambuko, ilikubalika kuwa Natembeya aongoze injili ya Sifuna magharibi mwa Kenya. Natembeya akakukabali na kuongoza mkutano nyumbani kwake Milimani, Kitale kuanza mchakato huo. Natembeya ni kiungo muhimu katika mkutano utakaomwidhinisha Sifuna kugombea Urais baadaye mwezi huu. Kiongozi huyo wa zamani wa kanda ya Rift Valley ana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko kutokana na athari zake za magharibi mwa Kenya. Kwanza, amefifisha umaarufu wa spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula. Hatua ya Natembeya kukubali kusimamia ajenda ya Sifuna inamsawiri kuwa mtu wa dhamira kubwa ya kuunganisha waluhya. Kwa umri, anamzidi Sifuna kwa miaka mingi tu lakini ameamua kumshika mkono mdogo wake. Wakosoaji wanashangaa sababu ya mkubwa kuonekana kuacha azma ya kuwa Rais kwa mdogo wake. Pili Natembeya ni gavana na ana eneo kubwa la usimamizi wa kaunti. Magavana huwa na uzito kushinda maseneta. Hivyo, ilitarajiwa na wengi kuwa ni Sifuna angemuunga mkono kwa sababu alikuwa ametangaza kuwa angegombea Urais. Tatu anatakiwa kufahamu kuwa safari ya umoja ya waluhya imekuwa ikikumbwa na changamoto za ubabe kati ya viongozi kutoka maeneo hayo. Safari hii alianza mwanasiasa mkongwe Masinde Muliro lakini aliyefaulu pakubwa alikuwa Michael Wamalwa Kijana katika uchaguzi mkuu wa 2002. Hivyo, Natembeya anatakiwa kuwa na mikakati zaidi ili kuvunja rekodi ya Wamalwa Kijana ambaye aliwaunganisha wenyeji wa magharibi mwa Kenya na kumpigia kura kwa fujo Mwai Kibaki na akawa Rais wa tatu wa Kenya huku Wamalwa akiwa makamu wake. Anapofanya hivyo anatakiwa kukumbuka kuwa Spika Wetangula hayumo katika usingizi, anataka Urais 2032. Mbunge Caleb Amisi amekuja na masharti yake kuhusu Linda Mwananchi. Paul Nabiswa ni mhariri, NTV
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.