WIRE โ JOHANNESBURG, Afrika Kusini: POLISI Afrika Kusini wamethibitisha kuwa kifo cha raia wa Nigeria korokoroni hakikutokana na maandamano dhidi ya wahamiaji wa kigeni nchini humo yaliyofanyika wiki jana. Maafisa hao wa usalama walisema kuwa mwanaume huyo aliaga dunia baada ya kuzirai kwa sababu alifumaniwa akiwa na dawa za kulevya ambazo inadaiwa alilenga kuiba. Wizara ya Masuala ya Kigeni ya Nigeria Jumapili ilidai kuwa raia huyo aliaga dunia wakati akihojiwa na polisi wa Afrika Kusini kuhusu tukio hilo. Iliongeza kuwa mahojiano hayo yalifanyika siku mbili baada ya maandamano makubwa dhidi ya raia wahamiaji haramu wiki jana. Maandamano hayo hasa yaliwalenga raia wasiokuwa na stakabadhi rasmi na yaliishia katika ghasia kwenye baadhi ya maeneo. Nigeria sasa imetishia kuchukua hatua ambayo haijaweka wazi iwapo raia wake wataendelea kuuawa Afrika Kusini. Nchi hiyo ni kati ya nyingine barani ambazo zimekuwa zikiwaondoa raia wake Afrika Kusini kutokana na kuhatarishwa kwa usalama wao. "Polisi Afrika Kusini inapinga vikali mwenendo na juhudi za kulinganisha tukio hili na maandamano dhidi ya wahamiaji yaliyofanyika wiki jana," ikasema taarifa kutoka Afisi ya Msemaji wa Polisi. Msemaji huyo alisema kikosi cha polisi kinachopambana na dawa za kulevya kilimkamata raia huyo wa Nigeria katika nyumba yake kufuatia operesheni iliyoendeshwa kutokana na taarifa za kijasusi. "Dawa za kulevya zilipatikana eneo la tukio, na mshukiwa alianguka ghafla alipokuwa akipelekwa rumande katika kituo cha polisi cha Pretoria," ikaongeza taarifa ya msemaji huyo wa polisi. "Wahudumu wa afya waliitwa na walithibitisha kuwa alikuwa amefariki dunia. Mamlaka huru inayosimamia uchunguzi wa mienendo ya polisi pia iliarifiwa na itafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo,"alisema msemaji huyo. Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini imesema serikali ya Nigeria inapaswa kuwasilisha ushahidi wowote ilio nao kuhusu kifo cha mwanamume huyo. Hata hivyo, serikali ya Afrika Kusini haijatoa maoni kuhusu madai ya dhibiti yaliyotolewa na serikali ya Nigeria. Maandamano dhidi ya wahamiaji kwa kiasi kikubwa yamekuwa ya amani, ingawa wakati mwingine yameishia vurugu, yakihusisha mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni na uporaji wa mali kwenye maduka yanayomilikiwa na wageni. Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema wageni wanasulubishwa tu ilhali serikali ya Afrika Kusini ndiyo ina wajibu kukabiliana na matatizo sugu kama uhalifu na ukosefu wa ajira. Vita dhidi ya Waafrika wenzao vimesababisha Afrika Kusini kuchukiwa na mataifa mengine barani na hata wengi walisherehekea timu yao ilipobanduliwa kwenye Kombe la Dunia.
"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."
This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.