WIRE โ€” MBUNGE Mwakilishi wa Kike katika Kaunti ya Mombasa, Bi Zamzam Mohamed na mwenzake wa Kwale Bi Fatuma Masito, wanakabiliwa na ushindani mkubwa kuelekea 2027 wakijaribu kuvunja mtindo wa jinsi wote waliowatangulia walivyohudumu kwa muhula mmoja pekee. Tangu uchaguzi wa kwanza wa mwaka 2013 chini ya Katiba iliyoleta ugatuzi, wapigakura wamekuwa wakichagua viongozi wapya kila baada ya miaka mitano. Katika kaunti ya Mombasa, Bi Asha Hussein ambaye alikuwa wa kwanza kushinda nafasi hiyo mwaka wa 2013 kupitia chama cha ODM, amekuwa akijitahidi kurudi mamlakani bila mafanikio. Alitumikia muhula mmoja kabla ya kushindwa na Bi Mishi Mboko mwaka wa 2017. Kwenye uchaguzi mkuu wa 2022, Bi Mboko aliamua kuwania ubunge Likoni na kufanikiwa. Hatua hii ilimpa nafasi Bi Mohamed kurithi kiti hicho. Katika Kaunti ya Kwale, marehemu Zainab Chidzuga alikuwa wa kwanza kushinda wadhifa huo 2013 lakini akashindwa na Bi Zuleikha Hassan mwaka 2017. Naye Bi Hassan alipoteza kiti hicho kwa Bi Masito wa ODM katika uchaguzi wa 2022. Bi Mohamed na mwenzake wa Kwale, Bi Masito, ambao wote ni wanachama wa ODM wameanza kuweka mikakati ya kubadili desturi katika kaunti zao. Bi Mohamed asema hana wasiwasi kuhusu uchaguzi ujao, akisisitiza kuwa kazi aliyoifanya ndiyo itakayomrudisha mamlakani. Alisema ataendelea kuwahudumia wakazi wa Mombasa na kwamba yuko tayari kugombea akiwa ndani au nje ya ODM, akidai kwamba kuna njama ya kumnyima tikiti ya chama. Aidha, ametangaza nia ya kuwania ugavana wa Mombasa baada ya kukamilisha kipindi cha miaka 10 kama Mbunge Mwakilishi wa Kike. Anakabiliwa na ushindani kutoka kwa kwa diwani wa wadi ya Kadzandani, Bi Fatma Kushe, mwanasiasa wa UDA, Bi Fatma Barayan, na mwanasiasa Amina Abdalla, huku wagombea wengine wakitarajiwa kujitokeza ifikapo hapo mwakani. Kwa upande mwingine, Bi Masito, ambaye amekuwa akiendeleza ziara za kiamendeleo mashinani, anatarajia pia kurejea mamlakani kwa msingi wa utendakazi wake. "Mimi watu wa Kwale nimewatembelea sana. Tushakubaliana na viongozi kwamba siasa hapa kwetu Kwale ni ODM," akasema, katika mkutano wa kuchangisha fedha za kuwezesha kina mama eneo la Matuga hivi majuzi. Wachanganuzi wa siasa wanasema mtindo wa wabunge wawakilishi wa kike kuhudumu kwa muhula mmoja pekee ni mzuri na unafaa kuigwa nchini, kwani wadhifa huo ulinuiwa kuwapa wanawake uzoefu wa kisiasa. "Hii nafasi ilitengewa wanawake ili waweze kuingia siasani, kupata tajriba au uzoefu, umaarufu, marafiki na fedha za kuwasaidia kugombea viti vingine vya kisiasa. Mwanamke hafai kusalia katika mamlaka hayo kwa zaidi ya miaka mitano. "Maliza miaka mitano upishe wanawake wengine ili tuweze kuhakikisha kuna wanawake wengi kwenye siasa," asema Bi Grace Oloo, mchanganuzi wa siasa. Bi Oloo pia aliwasihi wanawake kuwashikilia wenzao mikono ili kuwawezesha kisiasa.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.