WIRE โ€” TEHRAN, Iran: RAIA wa Iran Jumatatu, Julai 6, 2026 waliapa kuwa lazima nchi hiyo ilipize kisasi cha mauaji ya Kiongozi wa Kidini Ayatollah Ali Khamenei wakielekeza hasira zao kwa Amerika na Israel. Khamenei aliuawa mnamo Februari 28, siku ya kwanza ya Amerika na Israel kutekeleza mashambulizi dhidi ya Iran. Maelfu ya raia wa Iran walijitokeza katika msafara wa mazishi ya Khamenei yaliyofanyika viungani mwa jiji la Tehran. Msafara huo ulikuwa wa kumuaga rasmi kiongozi huyo wa kidini. Jumatatu ilikuwa siku kubwa zaidi katika wiki yenye shughuli nyingi za maombolezo. Picha za angani zilizorushwa na televisheni ya taifa zilionyesha maelfu ya waombolezaji wakiwa wamefurika katika barabara kuu katikati mwa mji wa Tehran. Majeneza ya kiongozi huyo aliyeuawa pamoja na jamaa wanne wa familia yake yalipelekwa, kupitia mitaa ya jiji hilo, kwa kutumia lori kubwa, huku magari ya wazimamoto yakinyunyiza maji kutoka juu ili kupunguza joto kwa waombolezaji. Msafara huo ulipopita chini ya daraja, waombolezaji walirusha mawe kuelekea bango lililokuwa limetundikwa juu likimwonyesha Rais wa Amerika Donald Trump akiwa amelengwa kwa risasi kichwani. "Amerika ilimuua baba yetu. Hatutawaacha mponyoke", likasema maneno kwenye bango hilo. Waombolezaji walikuwa wakipeperusha bendera za Iran pamoja na mabango mekundu. Mabango hayo yaliandikwa "walipiza kisasi wa Khamenei," ikiwa ni kauli yenye umuhimu mkubwa katika Uislamu wa Kishia tangu mjukuu wa Mtume Muhammad alipouawa vitani katika karne ya saba. Mnamo Jumapili, wana watatu wa kiongozi huyo aliyeuawa waliomba kando ya jeneza lake katika ukumbi mkubwa wa sala mjini Tehran. Hata hivyo, Mojtaba Khamenei, ambaye alimrithi baba yake kama Kiongozi Mkuu wa Iran, hakujitokeza hadharani. Inaaminika kuwa alipata majeraha yaliyomsababishia ulemavu wa uso katika shambulizi lililomuua baba yake. Tangu vita vilipoanza Februari 28 kufuatia mashambulizi ya anga ya Israel na Amerika dhidi ya Iran, Mojtaba hajaonekana tena hadharani. Shughuli za maombolezo zilianza Ijumaa wakati majeneza ya Khamenei mkubwa, mmoja wa mabinti zake na mtoto wake mwenye umri wa miezi 14, mmoja wa wakwe zake, pamoja na mke wa Mojtaba yalipowekwa kwa ajili ya viongozi wa Iran na wageni wa heshima kutoka mataifa mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho. Sherehe nyingine kubwa za maombolezo zilifanyika nje siku za Jumamosi na Jumapili kabla ya msafara mkubwa wa mazishi ya Jumatatu. Baadaye wiki hii, mwili wake utapelekwa katika misafara mingine ya mazishi katika mji wa Qom, ambao ni kitovu cha mafunzo ya Kishia n Iran, na pia katika miji miwili ya Iraq yenye maeneo matakatifu ya Kishia. Baada ya hapo utarejeshwa Iran kwa ajili ya mazishi katika eneo la kihistoria la makaburi ya Mashhad. Vita hivyo vilimalizika baada ya makubaliano ya awali ya amani yaliyofikiwa mwezi uliopita. Viliwaacha viongozi wa kidini wa Iran wakiendelea kubaki madarakani huku wakitangaza ushindi, na kudai kuwa wameongeza ushawishi wao kupitia udhibiti wa njia ya usafirishaji wa mafuta wa Strait of Hormuz. Trump pia amedai ushindi, ingawa malengo aliyoyataja mwanzoni mwa vita ya kuharibu uwezo wa Iran wa nyuklia na makombora, kuzuia uwezo wake wa kushambulia nchi jirani, na kuweka mazingira yatakayowawezesha raia wa Iran kuwaondoa viongozi wao madarakani, hayajatimia. Trump alisema mwishoni mwa wiki kwamba mazungumzo ya amani kati ya Amerika na Iran yameahirishwa kwa wiki moja kutokana na shughuli za mazishi. Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, alisema Jumatatu kuwa Khamenei mkubwa aliuawa kwa sababu aliongoza mpango wa kuiangamiza Israel. "Kiongozi yeyote wa Iran atakayejaribu tena kutekeleza mipango ya kuiangamiza Israel atauawa pia," akasema Katz.

"We aggregate wires to encourage regional discovery, sending readers directly back to the original source to explore full coverage."

This is a normalized overview of the breaking feed event. The complete, official release detailing all points, background context, and statements remains hosted by the original publisher.